Uongozi wa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba ulikuwa unatajwa kutaka kumfukuza kocha wao muingereza Dylan Kerr kutokana na kutofurahishwa kwa mwenendo wa timu hiyo hususani kupoteza katika michezo miwili dhidi ya Yanga na Tanzania Prisons.
Licha ya kuwa kitaalamu Simba
haikuwa imefanya vibaya sana katika mechi zake za Ligi Kuu maamuzi hayo
ya kutaka kumfukuza kocha yalikuwa yanawatatiza wengi, baadae stori
zikatoka kuwa kuna moja kati ya watu wa benchi la ufundi hupeleka maneno
ya kichonganishi kwa viongozi wa ngazi ya juu kuhusu Dylan Kerr.
Zote hizo zilikuwa stori tu
zinazoongelewa na watu na vyombo vya habari ila November 3 uongozi wa
klabu hiyo kupitia tovuti rasmi na account zake za mitandao ya kijamii
zimetoa majibu kuhusiana na mpango wa kumfukuza kocha Dylan Kerr, katika taarifa hiyo ambayo inatajwa kutoka kwa rais wa klabu hiyo Evans Aveva.
“Klabu
ya Simba na hususani uongozi wenu mara zote umeheshimu taaluma na
kujitahidi kuhakikisha kocha anafanya kazi yake bila kuingiliwa.
Tunaelewa wapenzi na wanachama wangependa tushinde mechi zetu zote, hili
pia ni tamanio la uongozi wa Simba”
“Lakini
kama ambavyo tulisema hapo awali kuwa ligi ya Tanzania bara msimu wa
2015/2016 itakuwa na ushindani mkubwa. Pia ni vizuri kuzingatia kuwa
hadi sasa Simba imecheza mechi nyingi nje ya Dar es Salaam ukilinganisha
na wapinzani wetu tena kwenye viwanja ambavyo msimu uliyopita tulipata
matokeo mabaya.Kwa niaba ya uongozi wa Simba napenda kuwapa taarifa
rasmi kuwa uongozi wenu uko nyuma ya kocha Kerr na tunampa sapoti kadiri
ya uwezo wetu”
CHANZO CHA HII STORI: simbasports.co.tz
Note: Only a member of this blog may post a comment.