Licha ya kuwa ana mashabiki wengi wa kike na anafanya muziki
unaowalenga zaidi mashabiki wa kike, staa wa Nigeria, Flavour N’abania
hafikirii kuoa na ametoa sababu zake za kuendelea kuwa mwanachama wa
chama cha mabachela.
Tumeshawasikia wasanii wengi akiwemo Davido wakitoa sababu za kwanini
hawajafikiria kuoa, lakini sababu aliyoitoa Flavour mwenye umri wa
miaka 31 ni kuwa hajaoa kwasababu hana muda wa kuwa na familia kwa sasa.
Akizungumza kwenye mahojiano exclusive na Myjoyonline, Flavour
amesema “Ndoa ni kitu kikubwa hivyo hutakiwi kukosea kufanya maamuzi,
hicho ndio kitu cha muhimu.”
Aliongeza kwa kusema “Kama unataka kuoa ilimradi kuoa basi itakuwa
haina maana, hauitafsiri maana ya ndoa, na kwasababu ya aina ya kazi
tunayofanya, hua nakaa nyumbani mara chache sana sasa nitapata wapi muda
wa kukaa na familia yangu? Ndio maana ni ngumu sana.”
Staa huyo ambaye ameshirikishwa kwenye hit song ya Diamond ‘Nana’
ameendelea kusema kuwa kama angekuwa anafanya kazi tofauti kama ya benki
au CEO wa kampuni ingekuwa rahisi zaidi kwake kupata muda wa
kutengeneza familia.
“Kwa karibia miezi miwili sasa sijakanyaga nyumbani, sasa kama
ningekuwa na mke nini kingetokea? Inamaanisha nisingeweza kwenda kazini,
ningepaswa kuwafikiria wao kwasababu siwezi kuwaacha wenyewe kiasi
hicho.” alisema Flavour.

Note: Only a member of this blog may post a comment.