Saturday, October 24, 2015

Anonymous

VIDEO: Baada ya Watu Kuzungumzia Tabia ya Utovu wa Nidhamu ya DIEGO COSTA, Hii Ndio Kauli Yake…

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Diego Costa ambaye amekuwa akiingia katika headlines kutokana na baadhi ya matukio yake anayoyafanya uwanjani, October 23 ameingia katika headlines tena baada ya kusema kuwa hawezi kubadilika kutokana na watu wanavyotaka na kufikiria. 

Diego Costa amekuwa akiingia katika headlines kutokana na vitendo vyake vya utovu wa nidhamu, Diego Costa tayari alishafungiwa mechi tatu mwaka huu katika vipindi viwili tofauti tofauti. Costa alifungiwa mechi tatu kutokana na kugombana na beki wa Arsenal Laurent Koscielny na kumkanyaga kwa makusudi beki wa Liverpool Emre Can.
Editorial use only. No merchandising. For Football images FA and Premier League restrictions apply inc. no internet/mobile usage without FAPL license - for details contact Football Dataco Mandatory Credit: Photo by Javier Garcia/BPI/REX Shutterstock (5111926bp) Diego Costa of Chelsea argues with Gabriel Paulista of Arsenal during the Barclays Premier League match between Chelsea and Arsenal played at Stamford Bridge, London on September 19th 2015 Barclays Premier League 2015/16 Chelsea v Arsenal Stamford Bridge, Fulham Rd, London, United Kingdom - 19 Sep 2015
“Sitobadilika hivyo kwa sababu ya watu wanavyoweza kufikiria, baadhi ya watu wanaweza kufikiria mchezo wa mpira wa miguu ni kama ukumbi wa michezo kuwa kila mmoja anaweza kufanya vizuri. Lakini nafikiria mtu hubadilika pale unapovuka mstari mweupe wa kuingia uwanjani na unakuwa mtu tofauti na pale unapokuwa nje ya uwanja, ila ninapokuwa uwanjani naenda kupambana kwa ajili ya timu yangu na kuhakisha nafanya vizuri”>>> Diego Costa
Hapa chini nimekuwekea video za matukio aliyowahi kufanya Diego Costa na kufanya afungiwe mechi tatu kwa kila tukio!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.