Saturday, October 24, 2015

Anonymous

VIDEO: Dereva wa Basi la Abiria Apoteza Fahamu Katikati ya Safari..Kilichotokea ni Hiki...!

Mara nyingi wasafiri huwa wanakuwa na imani yote kwa Dereva, wakati safari inaendelea unaweza kukuta abiria wanasinzia, wengine wako busy wanapiga story.. wengine wanachat, ni kwa sababu wana imani kwamba safari iko kwenye mikono salama ya Dereva.

Kuna wakati kumbe hata ajali zinatokea sio kwa sababu ya uzembe wa Dereva au ubovu wa gari, nimekutana na video kwenye mtandao wa Youtube.. Dereva kapoteza fahamu katikati ya safari Jiji la Guizhou China, kaanguka chini huku gari ikijiongoza yenyewe.

Basi lilikuwa na jumla ya watu kama 20 hivi, likaanza kuyumba ikabidi kijana mmoja aliyekuwa amekaa siti ya jirani asogee kwenye sterling kuingoza gari ili angalau isimame salama na kuepusha ajali.

Dereva wa Basi hilo alifariki wakati wakiwa njiani kumkimbiza Hospitali, lakini basi lilisimama salama na hakuna abiria yeyote aliyeathirika kwenye tukio hilo.
Video hii hapa ilirekodiwa kwa Camera ya CCTV ndani ya basi hilo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.