Hii itakuwa ni wiki nzuri sana kwa Vanessa Mdee ambaye weekend
iliyopita alifanikiwa kushinda tuzo ya Afrimma huko Dallas, Marekani
pamoja na kuachia wimbo mpya ‘Never Ever’ na video yake.
Vee Money ambaye amewashinda Victoria Kimani, Juliana Kanyomozi na
Khadija Kopa kwenye kipengele cha ‘Best Female East Africa’, ametoa
ushauri kwa wasanii wengine wa Tanzania kufata mifano waliyoionesha
yeye, Diamond pamoja na Ommy Dimpoz kwa kuwekeza kwenye muziki wao ili
wapate mafanikio.
Vanessa ambaye video yake mpya imefanyika Afrika Kusini na kuongozwa
na Justin Campos wa kampuni ya Gorilla Films, amesema, “Wasanii wengine
pia wachukulie mfano wa Diamond wa Ommy wa Vanessa wa kuwekeza kwenye
muziki wasiogope”
Pia amewashauri wasanii wa kike kujitokeza zaidi kutokana na uwepo wa
wasanii wachache wa kike kulinganisha na idadi ya wasanii wa kiume.
Vee pia amewashukuru wote waliomsupport hadi kushinda tuzo hiyo ambayo ni tuzo yake ya pili ya nje ya Tanzania

Note: Only a member of this blog may post a comment.