Katika vita vikali vya smartphones, washindani wawili wamepanga kuweka silaha chini.
Wenyeviti watendaji wa Sony na BlackBerry kwa nyakati tofauti wote
wamekubali kuwa mwaka 2016 unaweza kuwa mwaka wa kuachana na biashara ya
simu.
Sony imedai kuwa itafikiria mbadala mwingine kama kitengo chake cha
simu kitashindwa kuwapa faida, wakati BlackBerry ikidai haiwezi kusema
kuwa itafunga kabisa utengenezaji wa simu zao, japo mambo ni magumu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.