Camera za CCTV huenda zikarahisisha sana kazi ya Polisi kwenye kukusanya taarifa za ushahidi, jamaa mmoja alijikuta akimalizia hasira zake kwa Wafanyakazi wa kibanda kinachotoa huduma ya Internet baada ya kushindwa kwenye Kamali ambayo alikuwa anacheza Mtandaoni.
Jamaa huyo hajatajwa jina ila Video iliyonaswa na Camera za CCTV inaonesha kila kitu kuanzia alivyoanza kupasua Computer za Ofisi hizo mpaka anavyomshika na kumpiga mfanyakazi mmoja huku akidai kurudishiwa pesa yake Yuan 200 ambazo alitoa kununulia Kadi ya kuchezea game hiyo ya Mtandaoni… pesa hiyo ni kama Elfu 68 ya pesa ya Kitanzania.
Hiyo ishu imetokea Jimbo la Guiyang China na tayari Police wameanza kudili nayo kwa sababu jamaa kakamatwa tayari… anachodai yeye kisa cha kufanya hayo yote analalamika kwamba Kadi aliyopewa ilikuwa imekwisha muda wa matumizi kwa hiyo anachodai ni kurudishiwa pesa yake.
Wakati anafanya hayo yote alikuwa ameshika na kisu pia mkononi, hata ukiangalia kipande cha hii video inaonekana mfanyakazi huyo alipigwa lakini hakukuwa na mtu ambaye aliingilia kati kusaidia.
Tazama video hiyo hapa
Note: Only a member of this blog may post a comment.