HATA
kama utani, huu sasa umezidi. Kipa wa Simba, Manyika Peter jana asubuhi
katika mazoezi ya timu yake aliwatania wenzake kwa kuwaambia adhabu ya
Juma Nyosso imefutwa hivyo watakutana naye Oktoba 17, mwaka huu.
Nyosso, beki wa zamani wa Simba ambaye sasa ni nahodha wa Mbeya City, amefungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa muda wa miaka miwili na kutakiwa kulipa faini ya Shilingi milioni mbili kwa kosa la kumdhalilisha John Bocco wa Azam FC.
Kusikia hivyo, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Awadh Juma
akafikiria kisha akasema: “Duh! Inabidi tuvae pampasi (pampers) maana
jamaa yule hatabiriki.”
Awadh alisema licha ya vitendo vya udhalilishaji, Nyosso pia ni hodari wa kupiga viwiko (vipepsi) wachezaji wenzake pasipo kuonekana na mwamuzi na ukimrudishia unaonekana una makosa.
Abdi Banda yeye alisema: “Mimi akinigusa tutapigana sana maana siwezi kukubali kudhalilika kirahisi mbele ya watu, atanijua mimi ni nani na nitakachomfanyia ataacha tabia yake.”
Nyosso, beki wa zamani wa Simba ambaye sasa ni nahodha wa Mbeya City, amefungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa muda wa miaka miwili na kutakiwa kulipa faini ya Shilingi milioni mbili kwa kosa la kumdhalilisha John Bocco wa Azam FC.
Awadh alisema licha ya vitendo vya udhalilishaji, Nyosso pia ni hodari wa kupiga viwiko (vipepsi) wachezaji wenzake pasipo kuonekana na mwamuzi na ukimrudishia unaonekana una makosa.
Abdi Banda yeye alisema: “Mimi akinigusa tutapigana sana maana siwezi kukubali kudhalilika kirahisi mbele ya watu, atanijua mimi ni nani na nitakachomfanyia ataacha tabia yake.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.