STRAIKA Elius Maguli wa Stand
United ana mabao manane katika Ligi Kuu Bara na ndiye kinara wa
ufungaji, Kocha wa Simba, Dylan Kerr, amesema uwezo wa mchezaji huyo ni
aibu kwao.
Kabla ya kuanza kwa msimu huu wa ligi
kuu, Simba iliamua kuachana na Maguli ambaye amefunga mabao sawa na yale
ya timu hiyo, kwa madai kuwa uwezo wake ni mdogo uwanjani.
Kerr, raia wa Uingereza, aliliambia Championi Jumamosi kuwa, Maguli anastahili kupongezwa kwa kile anachofanya uwanjani na mafanikio yake ni aibu kwa Simba ambayo ilimuacha.
“Maguli anafanya vizuri kwa kufunga
mabao nane hadi sasa, ni aibu kwa Simba,” alisema Kerr na alipoulizwa
inakuwaje anasema aibu kwao wakati naye alishiriki kwenye kumuacha,
alisema:
“Kusema kweli ni yeye mwenyewe ndiye aliyetaka kuondoka Simba.”
Katika kikosi cha Simba anayeongoza kwa
ufungaji ni Hamis Kiiza aliyefunga mabao matano na wengine waliofunga
moja-moja ni Juuko Murshid, Joseph Kimwaga na Justice Majabvi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.