Picha hizo za mnato, zinamuonyesha El Fadhili akimtomasa kwa vidole vyake N’daw katika makalio yake wakati wa mchezo huo ambao Prisons ilishinda bao 1-0.
Muda mwingi wa mchezo huo, El Fadhili alionekana akimkaba N’daw na ni yeye aliyeshiriki kwa kiasi kikubwa kufichua hirizi iliyokuwa imevaliwa na straika huyo raia wa Senegal.
Championi Jumamosi lilipowasiliana na El Fadhili kuhusu kitendo chake hicho alisema; “Sikufanya kitendo hicho na sikumbuki hata kidogo, nadhani tuhuma hizo zinakuja ili kuzima aibu ya N’daw kukamatwa na hirizi.”
Kitendo cha El Fadhili ni mwendelezo wa vitendo visivyofaa vinavyofanywa na wachezaji wa ligi kuu katika michezo mbalimbali huku wa mwisho kufanya hivyo hivi karibuni akiwa ni Juma Nyosso wa Mbeya City aliyemfanyia John Bocco wa Azam.
Nyosso amefungiwa kucheza soka miaka miwili na faini ya Sh milioni mbili ikiwa ni mara yake ya pili kutenda kosa hilo kwani aliwahi kumfanyia Elius Maguli wakati anacheza Simba.
Endapo El Fadhili atapatikana na hatia, anaweza kufungiwa kucheza mechi zisizopungua tatu na hata faini ya fedha.

Note: Only a member of this blog may post a comment.