Jumatano iliyopita kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya akicheza dhidi ya Prisons, N’daw, raia wa Senegal, alizongwa na wachezaji wa timu pinzani kisha akakutwa na hirizi ambapo mwamuzi alimtoa nje kwenda kuitoa.
N’daw ameliambia Championi Jumamosi: “Sikukutwa na kitu chochote, ndiyo maana umeona nilikuwa nabishana na wale wachezaji, kama kuna kitu kimeonekana hakinihusu mimi.”
Pia, kwa mujibu wa kanuni namba 37 ya ligi kuu kipengele cha 7 (e), N’daw atafungiwa kucheza mechi tatu na kupigwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa hilo.
Kanuni hiyo inasema kuwa kufanya vitendo vyenye kuonyesha imani za kishirikina, uchawi adhabu yake itakuwa ni kufungiwa mechi tatu na faini ya Sh laki tano.

Note: Only a member of this blog may post a comment.