Sunday, October 4, 2015

Anonymous

Matokeo na Dondoo za Mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara Vipo Hapa (+Pichaz)

Mechi za Ligi Kuu soka Tanzania bara ziliendelea kama kawaida kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali Tanzania, licha ya kuwa kuna mechi tatu ambazo zimeharishwa kutokana na wachezaji wake wengi kuitwa katika kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na mchezo dhidi ya Malawi, October 3 imepigwa baadhi ya michezo ya Ligi Kuu.

Mechi ambazo zimechezwa Jumamosi ya October 3 katika viwanja mbalimbali Tanzania ni mechi ya Maji Maji FC dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Maji Maji Songea, Mwadui FC ambayo inanolewa na kocha Jamhuri Kiwelu imeibuka na ushindia wa jumla ya goli 1-0 dhidi ya mwenyeji wake Maji Maji FC.

Joram Mgeveke akipiga krosi ambayo Marcel Bonveture akijaribu kuzuia
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyofanikiwa kuona nyavu za mwenzake, dakika ya 56 kipindi cha pili Jabir Aziz akaiandikia goli Mwadui FC ya Jamhuri Kiwelu, goli ambalo lilidumu katika dakika zote tisini za mchezo na kuifanya Mwadui FC kuondoka na point tatu muhimu dhidi ya Maji Maji FC.

Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizopigwa October 3
Mgambo Shooting 0 – 0 Coastal Union

Benchi la wachezaji wa akiba wa Mwadui FC Nizar Khalfan wa kwanza katika benchi

Mashabiki waliojitokeza kuutazama mchezo huo

Watu wa usalama walikuwepo pia mtu wangu

Kocha wa Mwadui FC Jamhuri Kiwelu akitoa maelekezo

Waamuzi wa mchezo

Benchi la Maji Maji FC wakiwa pamoja na kocha wao Mika Lonnstorm

Jerson Tegete na wachezaji wengine wakishangilia kwa pamoja goli la Jabir Aziz

Zote hizi ni mbwembwe za vijana wa Julio wakishangilia goli la Jabir Aziz


Jerson Tegete ambaye alikuwa nahodha wa mchezo baada ya kutolewa na kwenda benchi


Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kutazama mchezo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.