Na Gladness Mallya
IKIWA kesho Jumapili ndiyo siku ya uchaguzi mkuu ambapo Watanzania wataamua nani awe rais wao, mastaa mbalimbali wamezungumza na Risasi Jumamosi kueleza walivyojiandaa na uchaguzi huu ambao unaonekana kuwa na changamoto nyingi kuliko nyingine zote zilizopita:
AMANDA POSHI
Uchaguzi wa mwaka huu ni wa tofauti sana
na zilizopita maana Watanzania wengi wana mihemko na hamu sana kutokana
na ushindani mzito uliopo, nimejiandaa vyema kikubwa tuombe uhai. Kura
yangu ni kwa Magufuli. Niwahusie Watanzania kwamba wazingatie sheria
zote za uchaguzi zilizowekwa ili kuepuka kuharibu kura zao.
Uchaguzi huu umejaa changamoto sana,
kuna upinzani mkali kuliko miaka yote, cha muhimu naomba amani itawale
jamani tukubaliane na matokeo yoyote yatakayotokea. Tukumbuke Tanzania
ni nchi yenye amani hivyo tusivurugwe na itikadi za vyama tukasahau
kwamba amani ni kitu muhimu kuliko kitu kingine chochote. Mtanzania
nenda kapige kura yako rudi nyumbani.
Mimi nimejiandaa vizuri lazima nipige
kura kwa sababu ni haki yangu ya msingi, uchaguzi huu umekuwa wa
ushindani sana kwa sababu vijana wameamka sana tofauti na miaka ya nyuma
tegemeo kubwa ni kuona mabadiliko. Kikubwa ninachomuomba Mungu ni amani
pia Watanzania tulizingatie hilo kwani tukiivuruga hatuwezi kuipata
tena.
Uchaguzi wa mwaka huu una changamoto
nyingi ni muhimu watu wakasikiliza sera zaidi maana watu wengi hasa
vijana wameibuka kuwa mashabiki wa vyama bila kujua sera za vyama
husika, yote kwa yote uchaguzi ni mgumu sana na utakuwa na matokeo ya
kushangaza mno. Jamani tumuombe Mungu atupitishe salama kwenye
hili maana wapo wanaofuata mkumbo wanaoweza kufanya vurugu zisizokuwa na
msingi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.