Saturday, October 24, 2015

Anonymous

KINGWENDU Kuchukua Maamuzi Haya Kama Akishinda Ubunge!

kingwendu 
Chande Abdallah
Mchekeshaji maarufu Bongo, Rashidi Mwinishehe ‘Kingwendu’ ameweka wazi kwamba yupo njiani kuachana na mambo ya uigizaji mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge.
Akizungumza na mwandishi wetu, Kingwendu ambaye anagombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Kisarawe kwa kupitia tiketi ya CUF, amesema kwamba kwa sasa kitu anachokifikiria ni kuwatumikia wananchi kupitia siasa. 

“Nimepanga kuachana na uigizaji, sitaki tena, ninatarajia kesho kuchaguliwa kuwa mbunge, ni mafanikio yangu na Bongo Muvi pia, hivyo sitaweza kuendelea na uigizaji, ninataka kuwatumikia wananchi kupitia siasa,” alisema Kingwendu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.