Mwandishi wa makala hii ni Ananilea Nkya ambaye ni Mkurugenzi Mstaafu wa TAMWA.
******
 
Watu wanaokampeni kushawishi Watanzania wamchague John Magufuli kuwa Rais wa tano wa Tanzania kwa kutumia kigezo cha uadilifu wanadhani ataweza kuzuia serikali ya CCM kuwa fisadi na hivyo umaskini wa wananchi kupungua.
Watu wanaokampeni kushawishi Watanzania wamchague John Magufuli kuwa Rais wa tano wa Tanzania kwa kutumia kigezo cha uadilifu wanadhani ataweza kuzuia serikali ya CCM kuwa fisadi na hivyo umaskini wa wananchi kupungua.
Kimsingi 
 wanajidanganya maana  Magufuli akichaguliwa  ufisadi  wa kimfumo 
unaofanywa na serikali ya CCM ili chama hicho  kibaki madarakani 
utaendelea kwa kasi na hivyo  pengo kati ya watawala wachache kutajirika
 kufuru   na mamilioni ya wananchi  maskini wa kutupa litaongezeka mara 
dufu.
Nchi
 yetu ilipopata uhuru maadui wa ustawi wa wananchi walikuwa ni 
watatu—adui mkuu ujinga—  na adui  wengine wawili  wanaotokana na 
ujinga—adui  umaskini na adui maradhi.
Lakini 
 katika zama hizi  za utandawazi  na demokrasia ya vyama vingi vya 
siasa  ameongezeka adui mwingine hatari nchini kwetu–adui  ufisadi.
  
Ufisadi  ameshamiri nchini baada ya mfumo wa vyama vingi vya siasa kuanza mwaka 1992.
Chanzo
 cha ufisadi  nchini  ni CCM kung’ang’ania madaraka  kwa kutumia nguvu 
ya fedha  na hivyo serikali yake kila inapochaguliwa   hugeuka kuwa 
fisadi na kuiba fedha  na mali za umma.
Hivyo,
 ikitokea  Magufuli akichaguliwa  wananchi wengi wataendelea kuwa 
maskini  kwa sababu inaelekea  Magufuli mwenyewe au hajui  au haamini 
kwamba chanzo  cha  umaskini  nchini ni serikali ya  CCM  kuwa fisadi  
na kuendekeza rushwa, ubabe, giliba, uongo na siasa za maji taka 
kushinda uchaguzi.
Inaelekea
 Magufuli hajatambua  kuwa kuzuia ufisadi unaozaa mafuriko ya wananchi 
maskini Tanzania kunahitaji  nchi iweke misingi ya kikatiba, lakini CCM 
kwa  kukataa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi  isiandikwe 
2014 iliikataa  misingi hiyo  kwa sababu  kinajua kinanufaika na udhaifu
 wa kikatiba uliopo sasa.
CCM
 inachofanya sasa ni Magufuli kuwapumbaza  wananchi kwamba  eti baada ya
 yeye kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, mafisadi  wameanza 
kuikimbia CCM.
Magufuli
 anataka  kuwaaminisha Watanzania kuwa  umaskini  unakabili mamilioni ya
 Watanzania  umesababishwa na wanaCCM walioondoka kwenye chama hicho 
baada ya yeye kuteuliwa kugombea Urais!
Pengine
 ndiyo sababu Magufuli  anaahidi kwenye kampeni zake kwamba akichaguliwa
 Rais  ataanzisha mahakama ya mafisadi kama alivyokaririwa kwenye 
mikutano yake ya  kampeni huko Dodoma.
Ninanukuu: ‘’Baadhi
 ya mafisadi wezi wameanza kukimbia baada ya CCM kuniteua mgombea urais 
lakini nikiingia Ikulu, nitawafuata huko waliko ili niwashughulikie 
vizuri ndiyo maana nimesema nitaunda mahakama ya mafisadi’’
Wananchi
 wanajiuliza kama ufisadi wa fedha  na mali za nchi unafanywa na 
serikali inayopewa  dhamana ya kuwa mlinzi wa fedha na mali za 
Watanzania endapo Magufuli atachaguliwa na serikali yake  kuunda 
mahakama ya mafisadi,  je majaji wa mahakama hiyo  watapata wapi ujasiri
 wa kumtia hatiani fisadi mkuu  (serikali) wakati kiongozi mkuu wa 
serikali  (Magufuli) ndiye atakuwa amewateua majaji wa mahakama hiyo?  
Je serikali inaweza kujihukumu yenyewe?
Aidha
 wananchi wanajiuliza   je  serikali  ya CCM imekuwa ikishindwa  
kuchukua hatua za kisheria kudhibiti  ufisadi wa  fedha na mali za umma 
unaofanywa na  serikali ya kwa vile nchi haina  mahakama maalumu ya 
kushughulikia kesi za ufisadi au ni kwa vile chama chao ni mnufaika wa 
ufisadi?
Wananchi wanauliza swali hili kwa sababu  ipo  mifano mingi  kuonyesha serikali ya CCM  ni fisadi .
Mfano wa kwanza:
 Ufisadi wa EPA kuiba kwenye  Akaunti ya EPA benki kuu jumla ya shilingi
 bilioni 133  mwaka 2005/6.  Wananchi walishangaa kuona Rais wa Jamhuri 
yetu  alivyopata kigugumizi  kwenye ufisadi huo.
  
Wananchi
 wanajiuliza  ilikuwaje mlinzi mkuu (serikali ya CCM) kama kweli  
haikunufaika na ufisadi wa  EPA haikuchukizwa na kitendo hicho cha aibu 
na kuchukua hatu za kisheria?
Kadhalika
 wananchi wanajiuliza, kama kweli wizi huo wa EPA haukuhusisha serikali 
yenyewe kunufaisha CCM ni kwa nini serikali ya CCM ilisema waliokwapua 
fedha hizo wamepewa muda wa kuzirejesha benki  na hadi leo (miaka 10 
baadaye) haijawatangazia Watanzania  hatma ya fedha hizo?
Mfano wa pili: Ufisadi
 wa Richmond. Kukotana na ukosefu wa umeme nchini serikali ya CCM 
iliingia mkataba na kampuni ya kigeni Richmond ili nchi ipate  umeme.
Kabla kampuni hiyo kuanza kuzalisha umeme zilitoka tuhuma kwamba Richmond  ilikuwa ni kampuni feki.
Wakati
 huo Edward Lowassa  alikuwa Waziri Mkuu,  kimamlaka hakuwa  Waziri wa  
Nishati, lakini aliamua kujiuzulu kulinda heshima ya serikali.
  
Lakini
 cha kushangaza baada ya kujiuzulu Lowassa  kampuni  ya Dowans 
iliyoirithi Richmond iliendelea kulipwa fedha nyingi kila mwezi hadi 
zikafikia bilioni 172.
Wananchi
 wanajiuliza  kama CCM  ilikuwa hainufaiki  na  mabilioni hayo 
yaliyokuwa yanalipwa  Dowans  na kwamba mnufaika wa ufisadi huo alikuwa 
ni Lowassa  ni kwa nini Dowans waliendelea kulipwa baada ya Lowassa 
kuachia ngazi? Ni kwa nini Lowassa hajafikishwa mahakamani hadi leo kama
 tuhuma dhidi yake zina ushahidi?
Wananchi
 wanajiuliza  kama CCM na serikali yake wanajinasibu  ni walinzi 
waaminifu wa  mali na rasilimali za Tanzania na kwamba wanastahili 
kuendelea kuajiriwa kuwa mlinzi mkuu wa fedha na mali za Tanzania baada 
ya uchaguzi tarehe 25 Oktoba mwaka huu 2015 ni kwa nini  serikali ya CCM
 ilipata kigugumizi kumpeleka  Lowassa mahakamani kumdai alipe hizo  
shilingi bilioni 172 kama kweli  ndiye aliyenufaika na ufisadi huo?
Mfano wa tatu: Ufisadi 
 wa  kuuza kwa bei chee  nyumba za Watanzania zenye thamani ya mabilioni
 ya shilingi huku  leo hii  serikali ikitumia fedha nyingi za umma  
kuwapangishia makazi  hotelini  watawala.
Wananchi wanafahamu kuwa  msimamizi  wa   uuzwaji wa nyumba  hizo ulifanyika  wakati  Magufuli akiwa na Waziri nyumba na makazi.
Karibu
 nyumba za umma elfu kumi ziliondoka mikononi mwa umma na hadi leo 
Watanzania hawajaelezwa zilipatikana shilingi ngapi kwenye mauzo ya 
nyumba hizo  na zilitumika kufanya jambo gani la kuwaondolea wananchi 
umaskini.
  
Aidha katika uuzaji wa nyumba za umma Magufuli anatuhumiwa  kuwauzia baadhi ya ndugu zake.
Wananchi
 wanajiuliza kama Magufuli na Lowassa wote walikuwa ni watendaji katika 
serikali ya CCM, na  wote  ufisadi umefanyika  kwenye maeneo ambayo 
walikuwa na dhamana,  ni kwa nini   leo  Magufuli anashabikiwa na CCM 
kuwa ni mwadilifu  ili hali  Lowassa akipakaziwa   ufisadi ?
Aidha,
 wananchi wanauliza  ufisadi   kwa Magufuli katika kusimamia kwa niaba 
ya serikali ya CCM  uuzaji kwa bei poa nyumba za umma umetoweka  kwa 
vile tu anagombea Urais kwa tiketi ya CCM na tuhuma za ufisadi kwa 
Lowassa mkataba wa Richmond umebaki kwa sababu tu ameamua kuondoka CCM 
na kugombea Urais   kwa tiketi ya CHADEMA –chama kinachowakilisha vyama 
vinne vya upinzani vinavyoundwa Umoja wa Katiba ya Wananchi-UKAWA?
Mfano wa Nne:
 Ufisadi wa Tegeta escrow 2014, serikali ya CCM ilifisadi bilioni 306.  
Watuhumiwa wa ufisadi huo walienea ofisi mbali mbali za serikali  hadi  
ofisi kuu  ya  ya  nchi –Ikulu  inayopaswa kuwa mahali patakatifu 
ilihusishwa na ufisadi huo!
Tena
 wananchi walielezwa jinsi mabilioni  ya  fedha hizo zilivyokwapuliwa  
kibabe  nyingine zikibebwa  kwa magunia na tandarusi mchana kweupe.
Watawala
 wa CCM waliopaswa kujiuzulu kama Lowassa alivyojiuzulu  na kisha 
kupakaziwa ufisadi tuliona jinsi walivyosafishwa  na serikali ya CCM 
yenyewe!
Wananchi
 wanajiuliza kama ufisadi wa Richmond haukuwa mkakati wa CCM wa kutumia 
siasa za maji taka kumtoa Lowassa  kafara wa ufisadi  kudanganya 
wananchi kwamba  serikali ya CCM siyo fisadi  bali fisadi ni Lowassa ni 
kwa nini   Magufuli  kwa dhamana yake kama Waziri wa Nyumba  alisimamia 
ufisadi wa  nyumba za umma  CCM inamuona mwadilifu na Waziri wa nishati 
 Muhongo  aliyekuwa na dhamana wakati wa ufisadi wa Tegeta escrow 
alisafishwa ili hali Lowassa   aliyesimamia ufisadi wa  mkataba wa 
Richmond  anapakaziwa ufisadi?
Zaidi
 wananchi wanajiuliza kama chanzo cha ufisadi  nchini kama vile Magufuli
 na CCM wanayotaka kuaminisha umma ni LOwassa na wengine walioondoka 
CCM,  je  ni kwa nini  serikali ya CCM imekumbwa na ufisadi wa Tegeta 
escrow  miaka saba baada ya Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu?
Hakika
 ziko fisadi nyingi  zilizohusisha viongozi wa serikali ya CCM  iwe ni 
kwenye miradi ya kitaifa au kwenye halmashauri  na  mikataba ya mali za 
nchi kama vile madini  kuonyesha kwamba  umaskini  wa wananchi 
unasababisha na  ufisadi wa serikali ya CCM.
Ndiyo 
 sababu  kwa kutumia mifano hii minne wananchi wanajiuliza  ni kwa 
nini   CCM imtoe  Edward Lowassa  kafara wa  ufisadi  ili  hali serikali
 ya CCM ndiyo fisadi?
Kadhalika
 wananchi  wanajiuliza ni kwa nini Edward Lowassa ambaye ameamua  
kuondoka CCM kutumia haki yake ya kikatiba  kutimiza ndoto yake ya 
kugombea Urais ,  CCM inamuona tishio na hafai kuwa Rais?
Kama
 alikuwa hafai kuwa Rais  kutokana na ufisadi ilikuwaje alipewa dhamana 
kubwa  ndani ya serikali ya CCM kuanzia uwaziri hadi Waziri Mkuu na 
akajiuzulu uwaziri mkuu ili kuzuia serikali ya chama chake isianguke 
kutokana na ufisadi?
Wananchi
 wanajiuliza hivi tatizo hapa ni ufisadi wa Lowassa kweli au ni CCM  
kutaka kung’ang’ania madaraka ya kuongoza  hata kama wananchi hawakitaki
 tena chama hicho kiongoze nchi?
Wananchi
 pia wanajiuliza hivi tatizo ni Lowassa ambaye anao uzoefu mkubwa wa 
kuongoza serikali na ambaye rekodi yake  inaonyesha kuwa ni mchapa kazi 
au tatizo ni  kwa vile anagombea   Urais kupitia CHADEM-UKAWA  na  
wananchi  wamemkubali ingawa CCM ilidhani umma ungemkataa kutokana na 
kuchafuliwa kimkakati   kwa  ufisadi?
Wananchi
 wanajiuliza  kama  Magufuli  ni mwadilifu  kuliko Lowassa na kwamba  
CCM  siyo inayonufaika na ufisadi unaofanywa na  watumishi wa serikali 
yake ni kwa nini CCM wamekataa kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni
 ya wananchi  ili kuweka misingi ya kikatiba kuziba mianya   kwa  
serikali ya chama chochote  kuwa fisadi wa fedha na mali za wananchi?
Wananchi
 wanajiuliza ni kwa nini CCM  inahaha  kumzuia Lowassa  kuwa Rais  wa 
Jamhuri  kama CCM  haiogopi   hatari ya kuachia chama kingine kuingia 
madarakani wakati nchi haijaweka misingi ya kuzuia serikali kuwa fisadi 
na hivyo wanaogopa kuwa  serikali ya CHADEMA  na UKAWA nayo itakuwa 
fisadi kama ilivyokuwa serikali ya CCM?
Vile
 vile wananchi wanajiuliza, kama Rais Jakaya Kikwete ambaye mwaka 2005 
alipigiwa kampeni na   CCM  kuwa ni mwadilifu, kama anavyonadiwa  
Magufuli sasa  lakini kwa miaka 10 umaskini wa wananchi umeongezeka 
–deni la taifa  limeongezeka kila Mtanzania  anatakiwa kulipa shilingi 
800,000/-—je Magufuli atakuwa na ubavu gani wa kuifanya CCM na serikali 
yake  isiendelee kuwa fisadi?
Ni
 kutokana na hoja hizi ndiyo sababu wananchi wengi wanaona kumchagua 
Magufuli kuwa Rais wa Tanzania ni kuchagua ufisadi na  ni kuchagua 
mamilioni ya watanzania waendelee na umaskini. HAIKUBALIKI.
Tena 
 wakati mamilioni ya wananchi wanaendelea kuwa maskini watawala wa 
serikali ya CCM, familia zao, wapambe wao kwenye kampeni na marafiki 
zao   wataendelea kujitajirisha kufuru na kwa kujigawia fedha na mali  
zinazopaswa kunufaisha Watanzania wote.
Ndiyo
 sababu wananchi sasa wanahamasishana kutambua kuwa kumchagua Magufuli 
ni kuichagua CCM na  ni kama  kumpa  tenda  ya ulinzi mlizi mwizi!
Wananchi
 wanaona ni afadhali kuichagua CHADEMA-UKAWA  kwa sababu kwanza mgombea 
 wake wa Urais  Lowassa  huenda akaonyesha uadilifu na uchapakazi  wa 
hali ya juu  kuwathibitishia Watanzania kwamba CCM amepakaziwa na 
kutolewa kafara ufisadi ili CCM iendelee kubaki madarakani bila 
kujulikana kwamba serikali yake ndiye malkia wa ufisadi nchini.
Wananchi
 wanatambua kuwa kuirejesha CCM  Ikulu   kasi ya  umaskini itaongezeka 
kwa wananchi wengi  kuaendelea kukosa  kipato, kukosa elimu bure na bora
 hadi chuo kikuu kuondoa adui ujinga na  wizi,  biashara chafu, uvunjifu
 wa haki za binadamu  na  serikali kuwa mbabe, dikteta mminya 
demokrasia  vitaongezeka na hivyo kuvuruga amani ya nchi yetu.
Hivyo  
 ni muhimu serikali ya CCM ikaacha sauti na maamuzi ya wananchi isikike 
katika uchaguzi mkuu  tarehe 25 Oktoba 2015  ili endapo  wananchi 
wataamua  kumchagua  Lowassa kama Rais wao kupitia CHADEMA  
inayowakilisha vyama vinavyounda   Umoja wa Katiba ya Wananchi 
(UKAWA),   waandike Katiba Mpya  inayotokana na maoni ya wananchi na 
wasipofanya hivyo uchaguzi wa  2010  wananchi wawanyang’anye madaraka.
Katiba
 mpya siyo tu  itampunguza madaraka ya Rais kuhusu uteuzi wa watendaji 
ikiwa ni pamoja na majaji wa mahakama, bali pia  itaweka misingi ambayo 
 mihimili  mitatu ya utawala wa nchi —Serikali, Bunge na Mahakama  
vitakuwa haviingiliani.
Kwa
 hivyo serikali ya chama chochote ikiiingia madarakani na ikafanya 
ufisadi itawajibishwa na wananchi nao wataacha na wizi na ujambazi wa 
kutumia silaha kujitajirisha kama watawala wao wanavyoiba fedha za umma 
kwa kutumia ujambazi wa kalamu.
Katiba
 Mpya ya wananchi ikiandikwa, serikali ikifisadi fedha na mali za 
wananchi itashtakiwa  na  majaji hawataogopa  kuihukumu serikali bila  
kuipendelea kwa sababu hawatakuwa na woga wa  kupoteza ajira.
Hayo
 ndiyo mabadiliko wanayotaka wananchi  wa Tanzania katika kukomesha 
ufisadi wa kimfumo ili kuepusha  ongezeko la wananchi masikini wa kutupa
 kunakohatarisha amani  na umoja wa  kweli  katika nchi yetu.
Lakini
 CCM na serikali yake vikitumia rushwa, ubabe na uchakachuaji  katika 
uchaguzi wa tarehe 25 na  kushinda uchaguzi, tuendako serikali ya CCM 
itafanya  ufisadi  mkubwa zaidi,  tena ikitumia  ubabe, udikteta na 
dharau kubwa kwa  vyama vya upinzani na wananchi kwa ujumla.  Mungu 
ibariki Tanzania.
Note: Ninaruhusu  yeyote anayetaka kutumia , kuchapisha au kusambaza andiko hili afanye hivyo.
------******------------******---------------------*********______
Mwandishi wa makala hii ni Ananilea Nkya ambaye ni Mkurugenzi Mstaafu wa TAMWA.
Anapatikana anapatikana kwa  E-mail:ananilea_nkya@yahoom.co


Note: Only a member of this blog may post a comment.