RAIS wa Tanzania anayemaliza
muda wake, Dk. Jakaya Kikwete ni kama amewaachia wosia wanasoka kwa
kusema kuwa kwa kiwango cha soka letu kilivyo sasa, kwa vyovyote vile
anahitajika mtu wa kazi ‘tingatinga’ ili kulifisha mbali zaidi.
JK alisema hayo jana kwenye kampeni za
Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Viwanja vya Jangwani ambapo alisema kwa
‘levo’ ya soka letu lilipofikia hasa timu ya taifa, Taifa Stars,
inayopambana kucheza Kombe la Afrika na lile la Dunia.
Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa, alisema
mtu pekee mwenye uwezo wa kuiwezesha Taifa Stars kufika hatua hiyo ni
Dk. John Magufuli ambaye ni mgombea wa urais kupitia chama hicho
anayeaminika kwa kupiga kazi.
“Nimejitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu
kuinua michezo nchini, lakini tulipofikia michezo yetu inahitaji mtu
tingatinga, mtu ambaye atatufikisha kucheza Kombe la Afrika na Kombe la
Dunia,” alisema JK.
Ikumbukwe kuwa katika miaka 10 ya utawala wake, JK amekuwa msaada mkubwa kwa kuwalipa mishahara makocha wa timu ya taifa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.