Friday, October 2, 2015

Anonymous

LOWASSA ATOA NJIA ZA SIRI NAMNA YA KULINDA KURA!


Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Bwana Edward Lowassa amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi ya Oktoba 25 kupiga kura na kuzilinda ili kuwezesha umoja wa katiba ya wananchi kuingia madarakani.

Akizungumza katika mkutano minee ya kampeni akianzia katika viwanja vya Mwembeyanga, Mhe. Lowassa licha ya kufurahishwa na idadi ya watu waliofika viwanjani hapo na kuahidi kumpigia kura za ndio ameelezea sababu ya kugombea uraisi na kuahidi akiingia madarakani atafanyakazi ya kazi ya kuwaletea maendeleo kwa kasi kubwa.
Waziri mkuu mstaafu Bwana Fredrick Sumaye ametaka wakazi wa Dar es Salaam kumpigia kura ya ndio mgombea urais Bwana Edward Lowaasa ili aweze kuingia madarakani ili aweze kurejesha sifa na maendeleo ya Tanzania pamoja na kuwaondoa watanzania katika lindi la umasikini.

Akizungumza katika mkutano wa pili wa kampeni uliofanyika Sinza Lowassa amewataka wakazi wa eneo hilo na maene ya jirani kuhakikisha wanampa kura za kutosha.

Aidha, Bwana Lowassa ametumia mikutano hiyo kuwanadi wagombea ubunge katika jimbo la Temeke, Kawe na Ubungo kupitia vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, ambapo wagombea walipata fursa ya kueleaza kero na matatizo katika maeneo hayo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.