Jada Pinkett-Smith akipozi kwa picha.
Jada Pinkett-Smith wakati akielekea ukumbini.
MWIGIZAJI na mfanyabiashara wa Marekani, Jada Pinkett-Smith jana alitokeleza vilivyo kwenye onyesho la wiki ya fasheni lililofanyika jijini Paris nchini Ufaransa.
Jada aliyekuwa amevaa nguo ya rangi ya dhahabu na nyeusi huku mguuni
akivaa viatu vyeusi aliwavutia mashabiki huku mapaparazi wakimzonga kwa
ajili ya kupata picha kutokana na mavazi yake hayo kumkaa vizuri na
kumfanya aonekane mrembo zaidi.
Jada ambaye ni mama wa watoto wawili, Jaden na Willow aliozaa na
mwigizaji Will Smith wiki mbili zilizopita alikuwa akisherehekea miaka
44 ya kuzaliwa kwake.
Note: Only a member of this blog may post a comment.