Sunday, October 18, 2015

Anonymous

Hivi Ndivyo Watu Walivyokesha Uwanjani Wakimsubiri LOWASSA, Hata Baada ya Kupigwa Mabomu Waligoma Kuondoka!

Hii ndiyo Tunduma bwana, Baada ya kusikia kwamba Lowassa, kipenzi na kiongozi wa Mabadiriko hapa Nchini atakuwepo hapa Tunduma leo hii mnamo kuanzia saa tisa alasiri, Wananchi wamekesha uwanja wa MAGEUZI (Zamani uwanja wa Dr Slaa) Shule ya Msingi Tunduma.

Polisi baada ya kusikia kwamba kunawatu wanakesha uwanjani, wakaenda kuwatawanya kwa Mabomu bila mafanikio, baadaye Viongozi wa Chadema wakaenda kuongea na Polisi na hatimaye wakafikia muafaka. hivyo kuwaruhusu watu kuendelea kukesha mpaka leo Asubuhi.
Kipande cha Barabara toka Kisimani mpaka Kanisani Roma, Kimepigwa Deki kinang'aa na kumeremeta kanakwamba ni Almasi mpya toka Dukani. Wafanyabiashara wanajiandaa kufunga Maduka yao ili kuhudhuria Mkutano huu wa Kihistoria ambao haujawahi kufanyika tangu Nchi yetu ipate Uhuru.

Uwanja wa Mageuzi unaonekana ni Mdogo, Kamati ya siasa ya Chadema inatakiwa kufika mapema ili kuwapanga watu ili kuzuia yale ya Tanga na Mwanza (Mungu Epushia mbali)
Kiufupi mji wa Tunduma Ulivyozizima.

BACK TANGANYIKA

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.