
Jenister Mhagama mgombea ubunge Jimbo la Peramiho akiwa katika kituo cha kupigia kura. Chekechea Namba 1, kijiji cha Parango
WAPIGA KURA wa majimbo ya Peramiho na Songea Mjini wamejitokeza kwa
wingi kwenye vituo vyao vya kupigia kura za Urais,Ubunge na Udiwani na
wengine wamekesha kwenye vituo vya misufini namba 1 na namba 2 vyao vya
kupigia kura kwa lengo la kuwahi foleni ya kupiga kura huku kasoro ndogo
ndogo zikijitokeza lakini bila kuathiri zoezi zima la upigaji kura
Akizungumza
na waandishi wa habari Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Peramiho ambaye
pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini, sisbert
Valentine Kaijage alisema kuwa waliojiandisha kwenye jimbo hilo ni
67,334 ambapo idadi ya vituo vya kupigia kura ni 195
Kaijage
alisema kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012
wilaya ya Songea Vijijini ina idadi ya wakazi 133024 na kwamba vifaa vya
kupigia kura vilishaperekwa kwenye vituo kwa wakati na changamoto
ambayo imejitokeza kwenye vituo hivyo ni baadhi ya watu ambao
walijiandisha kwenye majimbo ya uchaguzi wakiwemo wafanyakazi na
wanavyuo nao kutaka kupiga kura
Kwa
upande wake Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi Jimbo la Songea Mjini
Emmanuel Kibona kuwa kumejitokeza kasoro za Askari Mgambo kutokuwahi
kwenye vituo vya kupigia kura, baadhi ya wanasiasa kuvaa sare za vyama
vyao hali ambayo ilitaka kuleta taaruki, makarani kuendesha shughuli
polepole na kusababisha wapigakura kulalamika

Mgombea ubunge Songea mjini kwa tiketi ya CDM Joseph Fuime
Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kupiga kura kwenye
kituo cha Shuleni A kata ya Likuyufusi Mgombea Ubunge wa Chama cha
Mapinduzi Jimbo la Songea Mjini Leonidas Gama alisema kuwa ameridhishwa
na hali ya upigaji kura kwani umekuwa huru na haki
Gama
alisema kuwa tume imetenda kazi yake vizuri kwa kuhakikisha vifaa vyote
muhimu vya kupigia kura vimefikishwa kwenye vituo kwa wakati na
wapigakura wameanza muda muafaka kutumia haki yao ya kikatiba ya
kushiriki kupiga kura za ubunge, urais na Udiwani
Naye
Mgombea Ubunge wa Ccm Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama mara baada ya
kupiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Chekechea namba moja
kilichopo katika kijiji cha Parangu nje kidogo ya mji mdogo wa Peramiho
alisema kuwa anaamini kuwa wananchi wanaendelea kupiga kura bila kuwepo
kwa usumbufu wowote
Mhagama
alisema kuwa wananchi wameonyesha kuwa na imani kubwa na tume ya
uchaguzi kwani hakuna mahala ambapo kumekuwa na dosari kutokana na
uzembe au udhaifu wa tume hiyo hali ambayo inaendelea kuufanya uchaguzi
huo kuwa huru na haki
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Ruvuma
ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Said Thabit Mwambungu alisema kuwa mkoa
wa Ruvuma una majimbo 9 na kwenye majimbo yote 9 ya uchaguzi katika
mkoa huo vifaa vya kupigia kura vilipelekwa kwa wakati na wale wote
ambao walithubutu kuhujumu uchaguzi huo walichukuliwa hatua kali za
kisheria
Mwambungu
alisema kuwa katika Jimbo la Namtumbo kuna kata mbili uchaguzi wa
udiwani umeahirishwa kwa makubaliano na Tume ya Uchaguzi kutokana na
makosa yaliyojitokeza na wagombea wanafasi hizo kwenye kata hizo
wamekubali uamuzi huo na kwamba katika kata hizo kura ya ubunge na urais
zinaendelewa kupigwa huo
Note: Only a member of this blog may post a comment.