Monday, October 12, 2015

Anonymous

HABARI MBAYA Kwa Mashabiki wa Manchester City

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Manchester City, Sergio Aguero anatarajiwa kuwa nje kwa mwezi mmoja baada ya kupata jeraha nyuma ya goti lake wakati alipokuwa akiichezea Argentina.
Aguero alicheza kwa dakika 22 pekee wakati timu Argentina iliposhindwa na Ecuador. “Nadhani nitakuwa nje kwa kipindi cha mwezi mmoja,” Aguero aliiambia TYC Sport katika mji mkuu wa Bueno Aires.

Klabu ya Manchester City huenda itamkosa pia David Silva baada ya kuumia kutoka katika mechi ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Luxembourg baada ya kuteguka kifundo cha mguu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.