Jack Dustan.
Imelda Mtema
MWANADADA aliyejipatia jina
kupitia Shindano la Maisha Plus Season 11, Jack Dustan amejikuta
akiihama nyumba aliyokuwa amepanga maeneo ya Shekilango jijini Dar, kwa
madai kwamba ilikuwa na nguvu za kishirikina ‘mapepo’.
Akistorisha na Amani
hivi karibuni, Jack alisema nyumba hiyo alipanga na kukaa kama wiki
moja tu lakini akawa anakumbwa na mambo ya ajabu kwani kuna wakati
alikuwa akijikuta amelala nje kwenye kizingiti cha mlango wa chumbani
kwake.
Aliendelea kusema siku aliyoamua
kuondoka bila kubeba vitu vyake vya ndani ni baada ya usiku kupigwa sana
vibao na kuamriwa kutoa pombe alizoweka kwenye kabati ili awe salama.
“Ukweli sijabeba kitu chochote,
nilitimua zangu usiku uleule na kwenda kulala kwa rafiki yangu na
nimetafuta nyumba nyingine-,” alisema Jack.

Note: Only a member of this blog may post a comment.