Thursday, September 10, 2015

Anonymous

Habari Njema na Kubwa Zaidi Kwa SOKA la Tanzania Leo Ni Hii Hapa...

71
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (kushoto), akisaini mikataba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington kwa ajili ya michuano  hiyo , mapema leo katika Ukumbi wa  Kasenga uliyopo kwenye jengo jipya la Millenium Tower, Kijitonyama jijini Dar.
2
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington (kulia), akikabidhiana mkataba huo na Rais wa TFF, Jamal Malinzi kwenye uzinduzi huo.
3
Mkuu wa Masoko wa TFF, Simon Peter akisoma moja ya karatasi wakati wa kuchangua majina ya timu zitakazoshiriki mashindano hayo.
4-001
Mwenyekiti wa kamati ya ligi hiyo, Godfrey Nyange ‘Kaburu’, akielezea namna ligi hiyo itakavyoendeshwa hadi kupatikana kwa mshindi.
5
Mwakilishi wa vilabu vinavyotarajiwa kushiriki katika mashindano hayo, Eli Mzozo akitoa neno la shukrani kwa TFF na Azam kwa kuanzisha mashindano hayo.
6
Jamal Malinzi akijibu maswali yaliyoulizwa na baadhi ya waandishi waliokuwa kwenye uzinduzi huo.
7
Wadhamini na wasimamizi wa ligi hiyo wakiwa kwenye picha ya pamojna muda mfupi baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo.
8
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa ligi hiyo.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ushirikiano na Azam Media Ltd. limetangaza uzinduzi wa shindano jipya litakaloitwa “Azam Sports Federation Cup”.

Shindano hili ambalo laweza kufananishwa na mashindano ya baadhi ya nchi za Ulaya na kwingineko kama vile FA Cup ya England na Copa del Rey ya Hispania , litaendeshwa kwa mfumo wa mtoano na kushirikisha timu mbalimbali si tu za Ligi Kuu ya Vodacom, bali pia nyingine kutoka madaraja mengine mawili ya chini na kufanya idadi ya timu kuwa 54 .

Mfumo huu una msisimko wa aina yake huku ukitoa fursa kwa timu ya daraja la chini kuitupa nje ya mashindano timu ya daraja la juu au maarufu.

Azam Media imepata haki ya udhamini na matangazo ya shindano hili muhimu kwa kipindi cha miaka minne.

Ratiba ya mzunguko wa kwanza imefanyika wakati wa mkutano wa waandishi wa habari ambao ulioneshwa moja kwa moja na Azam TV. Mizunguko mingine ya shindano hili itapangwa katika tarehe ambazo hakuna michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom ili kuwawezesha mashabiki wa kandanda kufaidi uhondo wa mchezo huu kwa kipindi chote cha mwaka.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington amezungumzia uzinduzi huo: “Huu ni wakati muhimu kwa wapenzi wa kandanda hapa Tanzania na pia ni mapinduzi ya matangazo ya luninga.

Nimekuwa nikisema mara zote kuwa lengo letu ni kuufanya mchezo huu kuwa sehemu nzuri ya burudani kuliko shindano linalomalizika ndani ya muda mfupi.” Alipoulizwa kuhusu jina la shindano hilo amesema: “Limekuwa jambo zuri kuwa shindano hili jipya litabeba jina la chaneli yetu ya Azam Sports ambayo inatoa fursa kwa watazamaji kuona pia michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom, La Liga na sasa michezo ya ASFC moja kwa moja katika picha ang’avu zaidi.

Pamoja na makubaliano ya karibuni ya kuwa mshirika rasmi wa TFF kwa matangazo ya michezo ya kimataifa ambayo wana haki, hatua hii inaimarisha uhusiano wa pande mbili hizi kwa manufaa ya michezo hapa Tanzania”.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameeleza matumaini yake juu ya shindano hilo jipya: “Kwa muda mrefu nimekuwa nikihitaji Tanzania kuwa na aina yake ya Kome la FA na sasa, kwa kuungwa mkono na Azam Media, siku hii imewadia.

Uzoefu wa kufanya kazi nao kwa zaidi ya miaka miwili sasa na kufanya VPL kuonekana kwa mashabiki nchini kote umedhihirisha kuwa ni washirika muhimu, na wana dhamira kama ya TFF ya kuboresha kandanda la Tanzania kadiri iwezekanavyo”.
(Habari/Picha: Musa Mateja na Denis Mtima/GPL)

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.