Mitandao ya kijamii imekua ikitumika sana pia wakati huu wa kampeni
kueleka kwenye siku kubwa ya Wananchi kufanya maamuzi ya nani aichukue
nchi hii kwenye awamu ya tano kama Rais ambapo vyama viwili vilivyobeba
headlines za Urais kwa uzito vikiwa ni CCM na CHADEMA kwenye UKAWA.
Kingine ni kwamba vyama hivi vimeona umuhimu wa mitandao ya kijamii mpaka Wagombea wao kuwa na account za Twitter ambazo ni Verified yaani zimethibitishwa na Twitter wenyewe kwamba ni Account halali za Wanasiasa hawa.
Mpaka September 20 2015 page ya Twitter ya Edward Lowassa ilikua na Wafuasi zaidi ya elfu 21 na ya Dr. John Pombe Magufuli zaidi ya elfu 23 ambapo haya hapa chini ni mambo sita kutoka kwenye kila page.

Note: Only a member of this blog may post a comment.