Mgombea uras kwa tiketi ya ACT – Wazalendo, Bi. Anna Mghwira amesema kuwa Tanzania imekosa viongozi bora wanaoweza kuiletea maendeleo makubwa licha ya kuwa na utajiri mubwa wa maliasili.
“Watu wanaojua na wanaoguswa na matatizo ya watu ndio wanaopaswa kuliongoza taifahili ambalo kwa miaka 50 limekuwa likiburuzwa na viongozi ambao wanajigamba kuwa wamelibadili kwa maisha bora,” alisema huku akiwataka wananchi hao kumchagua yeye na chama chake ili kuleta mabadiliko ya kweli.
Aliahidi wananchi hao kuwa endapo watampa ridhaa ya kuiongoza Tanzania atahakikisha wananchi wa Katavi wanapata ajira kutokana na misitu ya eneo hilo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.