Saturday, September 12, 2015

Anonymous

Maandishi Ya Mkono Ya Marehemu TUPAC SHAKUR Akiwa Jela Kuuzwa Mamilioni!

Mashairi yaliyoandikwa kwa mkono ya Tupac Shakur akiwa gerezani ya ‘Ambitionz As A Ridah’ yaliyoandikwa kwenye karatasi mbili tofauti yatapigwa mnada na kumilikishwa kwa mtu yoyote.


Kwa mujibu wa ITV ya Marekani, mashairi hayo aliyoyaandika akiwa jela mwaka 1995 yatapigwa mnada mwishoni mwa mwezi huu jijini London, Uingereza. Yanatarajiwa kuuzwa kati ya $47,000 na $78,000.
‘Ambitionz Az A Ridah’ ilitumika kama utangulizi wa album ya nne ya Tupac ‘All Eyez on Me’ iliyokuwa album ya mwisho kabla hajauawa kwa risasi mwaka 1996. Album hiyo iliwashirikisha wakali kama Snoop Dogg na Dr Dre.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.