Kim Davies aliyetupwa jela kwa kutosaini cheti cha ndoa.
JAJI mmoja nchini Marekani, ameagiza
ofisa mmoja wa serikali katika Jimbo la Kentucky, kufungwa jela, baada
ya kukataa kutekeleza agizo la mahakama la kutoa cheti rasmi cha ndoa,
kwa wapenzi wawili wa jinsia moja.
Kim Davies amesema imani yake kama Mkristo, haimruhusu kusaini cheti kama hicho.
Ndoa ya jinsia moja ilihalalishwa nchini Marekani Juni mwaka huu.
Wananchi wanaounga mkono ndoa za jinsia moja wakiwa nje ya mahakama.
Uamuzi huo wa Davis, wa kutosaini cheti hicho umepokelewa kwa hisia tofauti.
Kuna baadhi ya wale wanaomuona kama shujaa huku wengine wakisema ni msaliti.
Kuna baadhi ya wale wanaomuona kama shujaa huku wengine wakisema ni msaliti.
Davis ambaye ni karani wa mahakama, alikataa kutoa cheti hicho, kwa wanandoa hao katika Wilaya ya Rowan iliyoko Kentucky.
Ofisa huyo ambaye alichaguliwa na raia amesama, kitendo hicho kinakiuka maadili ya kidini.
Davis sasa ametupwa jela na jaji huyo kwa kuidharau mahakama.
Amesema alikuwa amekula kiapo cha kuwa ofisini na viapo vina maana nyingi.
Amesema alikuwa amekula kiapo cha kuwa ofisini na viapo vina maana nyingi.
Watu wanaoshabikia ndoa ya jinsia moja,
walikusanyika nje ya mahakama, wakiimba kuwa mapenzi yameshinda na
kusema kuwa sasa wanafuraha kwa sababu wanaweza kufunga ndoa.
Lakini kwa upande wake Kim Davis amepata
uungwaji mkono kutoka kwa Wakristo wahafidhina na baadhi ya wagombea wa
urais wa Chama cha Republican, ambao wanasema kuwa Davis amehukumiwa
jela kwa kufuata imani zake.

Note: Only a member of this blog may post a comment.