Faiza Masaka
Paga (23) mkazi wa Chanika, Msumbiji, Wilaya ya Ilala jijini Dar, ambaye
alikuwa akisumbuliwa na uvimbe kwa muda mrefu hatimaye amefanyiwa
upasuaji na madaktari bingwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wiki
iliyopita.
Faiza
aliliambia gazeti hili kuwa kutokana na kufanyiwa upasuaji kwa
mafanikio makubwa, alitolewa uvimbe uliokuwa na kilo sita na nusu
mwilini mwake.
Alisema
anawashukuru wananchi wote waliomchangia fedha baada ya kuandikwa
habari yake katika gazeti hili tolea namba 915 la Juni 23 hadi 25 mwaka
huu likiwa na kichwa cha habari: GONJWA LA AJABU, hali iliyosababisha
wananchi kujitokeza kwa wingi kumchangia.
Faiza ni yatima sasa anauguza kidonda,
anasaidiwa na msamaria mwema mwanamke ambaye ana kipato cha chini
isitoshe ana watoto wawili ambao afya zao siyo nzuri.
Pia
bado anatakiwa kwenda Hospitali ya Muhimbili kila wiki mara moja
ambapo anatakiwa kukodisha teksi kwenda na kurudi lakini fedha hana.
Kwa yeyote anayependa kumsaidia binti huyu awasiliane naye kwa namba ya simu : 0787 853153, 0654 187240 au 0717 260769.

Note: Only a member of this blog may post a comment.