Gabriel Ng’osha na Gladness Malya
NDIYO maana! Mtabiri
bingwa na mtaalam wa nyota Afrika Mashariki Maalim Hassan Yahya amepasua
jipu kuwa wagombea wawili wa urais katika uchaguzi wa mwaka huu, John
Magufuli na Edward Lowassa wanabebwa na nyota zao.
Akizungumza na waandishi wetu hivi
karibuni, alisema kinajimu, herufi M inayosimama badala ya Magufuli,
nyota yake ni ya samaki ambayo asili yake ni maji wakati herufi L kwa
maana ya Lowassa, nyota yake ni mshale, ambayo kiasili ni moto na ndiyo
maana kuna mvutano mkubwa sana katika uchaguzi wa mwaka huu.
“Maji yana nguvu kubwa sana ya kuweza
kuuzima moto kama yakimwagikia vizuri huo moto, lakini pia moto nao
unaweza kuyafanya maji yakachemka mpaka yakakauka na kuunguza sufuria,
hivyo duru ya siasa za mwaka huu chochote kinaweza kutokea,’’alisema
Maalimu, mtoto wa mnajimu mashuhuri wa zamani, Sheikh Yahya Hussein.
Hata hivyo, Hassan ameitaka serikali na
vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama kuwa makini katika uchaguzi wa mwaka
huu kutokana na viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyoanza kujitokeza
nchini.

Note: Only a member of this blog may post a comment.