NI Jumanne
tena! Naamini wasomaji wangu wote mpo sawasawa na tayari kupokea mada
mpya ya wiki hii. Habari kubwa ya kitaifa kwa sasa ni siasa, kampeni za
wagombea na vishawishi vyao. Lakini najua bado hamkosi elimu ya mapenzi
na maisha.
Leo nataka kuwasaidia baadhi ya
wanawake, hasa wasichana ambao wamejikuta wakiwa kwenye uhusiano
usiodumu kwa sababu ya kuwapata wanaume wanaowatamani halafu wao kwa
kutokujua, wakaamini wanapendwa.
MAPENZI YALIVYO
Awali ya yote napenda kueleza kuwa,
mapenzi yana hisia, yanagusa, yanagharimu. Wawili wanapotokea kupendana
ndiyo huitwa mapenzi na si mmoja kupenda mwingine asipende. Huko ni
kudanganyana.
HALI ILIVYO
Lakini sasa kuna wanaume wanaopenda na
wapo wasiopenda. Ila wanatamani. Mbaya zaidi kundi hili la wanaume
wasiopenda bali wanatamani, hata wenyewe hawajijui kama hawajui kupenda.
Baadhi ya wasichana wamekuwa
wakilalamika kupigwa chini na wanaume. Tena wanasema hupatwa na kitendo
hicho baada ya kukutana kimwili na wanaume hao mara moja au mbili.
Msikie Jamila, mkazi wa Tandale, Dar:
“Mimi najiona nina mkosi. Mwanaume
ananionesha ananipenda sana, nami najitoa kwake. Lakini akishalala na
mimi mara moja au mbili, anaingia mitini. Hapokei simu, hajibu meseji.
Nisaidie anko Ndauka.”
KUNA HILI
Nisiseme tu kwamba tatizo la Jamila
linatokana na kupata mwanaume anayetamani, lakini pia inawezekana
‘uwezo’ wake kwenye sita kwa sita unachangia. Wapo wanaume wakiona
mwanamke ‘hajiwezi’ uwanjani, anamkimbia. Yaani mwanamke anakuwa hana
sifa ya kumshika mwanaume.
TURUDI KWENYE MADA
Hata hivyo, sasa turudi kwenye mada yetu ya leo; sifa tano za mwanaume anayekutamani.
KUTODUMU NA MWANAMKE
Sifa ya kwanza ya mwanaume mwenye tabia
hii ni kutokudumu na wanawake. Utakuta mwanaume ana mpenzi, baada ya
mwezi mmoja wamemwagana, anakuwa na mwingine. Wapo wasiodumu na wapenzi
wao hata kwa mwezi mmoja.
KUKINAI TENDO LA NDOA
Sifa ya pili ya mwanaume mwenye tabia
hii ni kukinai tendo la ndoa. Hapa namaanisha kuwa, mwanaume mwenye
tabia ya kutamani huwa hawezi kukutana kimwili na mwanamke zaidi ya mara
tatu. Anakuwa ameshamkinai na hamtaki tena. Chenga nyingi. Wako
wengine, wenye sifa hii, akishamnasa mwanamke akalala naye mara moja tu,
basi! Tena wengi wao wanapenda kuhifadhi kumbukumbu.
Utakuta mwanaume anakuhesabia wanawake
aliokwisha lala nao; Ester tayari, Jamila tayari, Jane pia, Suzana yeye
juzijuzi tu. Halima zamani, Hawa tayari, sasa hivi namfukuzia Maimuna.
Mwanaume wa hivi, anajua kutamani lakini si kupenda
Itaendelea toleo lijalo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.