Hitmaker wa Shikorobo, Shetta amekanusha kubebwa na wasanii anaofanya
nao kolabo na kwamba nyimbo anazofanya mwenyewe hazifanyi vizuri.
Shetta ameiambia Bongo5 kuwa nyimbo zake nyingi alizowashirikisha wasanii wengine yeye ndio amekuwa akifanya kazi kubwa.
“Mimi naamini ngoma kama Shikorobo nimeimba chorus mwenyewe na verse
mbili mwenyewe,” amesema. “Ningekuwa nimemtoa pia ningefanya vizuri.
Kcee amekuwepo kwa sababu ni international artist ili kufanya kubwa
zaidi Nigeria, pia yeye anakuhitaji huku na mimi nakuhitaji kule.
Kwahiyo amenitumia mimi na mimi nimemtumia yeye.”
“Maneno kama hayo hayaniumizagi as long as nafanya kazi nzuri na ngoma zangu nyingi kazi kubwa nafanya mimi,” amesisitiza.
-via Bongo5

Note: Only a member of this blog may post a comment.