Bado matukio ya watu kupoteza maisha kutokana na upigaji wa picha za Selfie yameendelea kuripotiwa kila siku.
Hii nyingine ni mwendelezo wa matukio hayo ambapo huko Russia kuna
mwanafunzi mmoja kawachukua marafiki zake na kutaka wamsindikize kwenda
kupiga selfie ya kipekee kwenye moja ya majengo marefu nchini humo.
Walipofika mwanafunzi huyo akapanda juu ya jengo hilo lenye gorofa
tisa na akaanza kupiga picha ili atimize lengo lake la kupiga selfie ya
kipekee.
Sekunde chache baadaye aliteleza na kudondoka chini ambapo
alikimbizwa hospitali akiwa na majeraha makubwa na baada ya masaa mawili
kupita alifariki dunia.
Note: Only a member of this blog may post a comment.