Mastaa wa muziki wa Afrika Diamond wa Tanzania, Davido wa Nigeria na
rapper AKA wa Afrika Kusini wameshare picha za kudhihirisha ni jinsi
gani wanajivunia kuwa ‘baba’. Mastaa hao wote watoto wana watoto wa kike.
Rapper AKA ambaye hivi karibuni ametengana na mama wa Mwanaye DJ
Zinhle ameshare picha akiwa amembeba mtoto wake kwa hisia na kuandika
“Real stuff.“
Davido alishare picha ya mtoto wake na kuandika “AURORA DABBIN ON EM!! #BILLIONAIREBABY”.
Diamond Platnumz ambaye amekuwa akionesha mapenzi mazito kwa binti
yake Tiffah toka amezaliwa, ameshare picha mpya akiwa amempakata mwanaye
ikiwa ni siku chache kabla ya tarehe ya kumuonesha sura kwa mara ya
kwanza Septemba 20.

Note: Only a member of this blog may post a comment.