Friday, September 4, 2015

Anonymous

PICHAZ: Mama DIAMOND na mama ZARI walipokutana kwenye ‘state house’ ya PLATINUMZ

Nyuso za wazazi wa mastaa wawili wa Afrika, Diamond na Zari zilionekana zenye furaha mbele ya mjukuu wao Lattifah Nasib a.k.a Tiffah katika picha waliyopiga nyumbani kwa Diamond ambapo mwenyewe anapaita ‘state house’.
Zari amepost picha ya mama yake mzazi akiwa amembeba Tiffah na pembeni akiwa na mama yake Diamond, kwa pamoja wanaonekana wakizungumza jambo kwa furaha huku wakicheka.
Kwenye picha hiyo Zari aliandika;
“Good morning, let’s take this opportunity to comment with a prayer for our parents. And those who’ve lost your parents, my heart is with you. Comment with a prayer for the good Lord to rest them in peace. This is mama Zee and mama Dee”
Bila shaka furaha za wazazi hao wa kike zitakamilika pale Diamond na Zari watafunga ndoa na kuziunganisha familia zao.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.