Mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke.
Wilbert Molandi, Dar es Salaam
WAKATI Yanga ikionekana kama imekuwa na tatizo la wapigaji wa penalti kutokana na mwenendo wao wa hivi karibuni, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Deus Kaseke ameomba abebeshwe jukumu hilo kwa kuwa anajiamini anaweza, hivyo kama akipewa yeye ndiye atakuwa mfalme mpya wa kupiga penalti klabuni hapo.
Yanga ilifungwa na Azam FC katika Kombe la Kagame kwa penalty, pia ilishinda kwa penalti dhidi ya Azam haohao katika Ngao ya Jamii lakini ilipofika hatua hiyo ya kupigiana mikwaju hiyo, ilionekana wazi mashabiki wa Jangwani hawana imani na timu yao hiyo.
“Mimi sina hofu kabisa katika penalti, tangu nimeanza kupiga sijawahi kukosa kwenye mechi za ushindani. Ikitokea nikapewa jukumu hilo naamini lazima nitafunga.
“Penalti yangu ya kwanza kupiga nikiwa Yanga ni ile ya Ngao ya Jamii ambayo niliifunga kwa kumchambua kipa,” alisema Kaseke.

Note: Only a member of this blog may post a comment.