Brighton masalu
‘MTOTO laini’ katika
kiwanda cha ‘kusindika’ filamu Bongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amesema
miongoni mwa mambo ambayo kamwe hayafanyii mzaha ni pamoja na kuruhusu
mwili wake ‘uguswe’ kwa urahisi na wanaume wakware.
‘Akibananishwa ukutani’ na ‘kisabengo’
wetu kwa maswali magumu juu ya kutoonekana hadharani au kumwanika
mwandani wake hivi karibuni, Odama alisema yeye ni mwanamke thabiti
aliyelelewa katika maadili halisi ya kiafrika, hivyo suala la kuwa na
mwanaume halihitaji ‘promo’ kwani ni kawaida kwa mtu mzima aliyekamilika
kuwa na mwenzi, huku akiweka bayana kuwa mwili wake si sadaka hivyo
haguswi kirahisi.
“Kwani kuwa na mwanaume ni fasheni?
Nimelelewa na familia yenye maadili ya kiafrika, suala la kuwa na
mwandani si biashara wala matangazo, kwa hiyo nikiwa naye si lazima kila
mtu ajue au amjue, kwanza mimi si mwanamke rahisi, mwili wangu hauguswi
hovyo na wanaume wakware, unanionaje? Najielewa na kujitambua,” alisema
Odama.

Note: Only a member of this blog may post a comment.