Jamaa mmoja mume wa mtu aliyetambulika kwa
jina la Geofrey mkazi wa Geita amejikuta akishushiwa kipigo cha kufa mtu
na majirani zake baada ya kumpiga mkewe nusu kufa bila sababu za
msingi.
Akizungumza na paparazi wetu, mpashaji wetu kutoka eneo la tukio
alisema kuwa awali Geofrey ambaye ni mlevi maarufu mtaani hapo, alikuwa
na tabia ya kumshushia kipigo mkewe mara kwa mara kila anaporudi kutoka
kilabuni bila kujali hali mbaya ya mkewe ambaye ana kichanga cha miezi
miwili.
Mpashaji wetu anasema kuwa, siku ya tukio Geofrey kama kawaida yake
alifika nyumbani kwake usiku wa manane akiwa ‘ameutwika’ na kumtaka
mkewe amfungulie mlango. Baada ya kumfungulia kama kawaida yake
alimvamia na kuanza kumshushia kipigo mfululizo hadi akazimia jambo
lililowakera majirani zake ambao waliamua kumshushia kipigo cha mwizi
Geofrey wakidai wameichoka tabia ya kumpiga mkewe hivyo wanampa onyo.
“Ndiyo tabia yake yaani unakuta anampiga mkewe usiku wa manane tena
huku akimtukana, sasa juzi ndiyo akakutana na wanaume wenzake
wakamnyoosha unaambiwa siku hizi mbili naona katulia heshima ipo kwa
mkewe,” alisema mpashaji wetu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.