Thursday, September 17, 2015

Anonymous

PENNY Aangua Kilio Hadharani BSS

PENNY1.jpgImelda Mtema

MTANGAZAJI matata wa Bongo Star Search (BSS 2015),   Penniel Mungilwa ‘Penny’ wiki iliyopita alijikuta akiangua kilio bila aibu baada ya majaji wa shindano hilo kutaja washiriki waliokuwa wakiaga. 

Akipiga stori Amani, Penny alifafanua sababu ya kushindwa kujizuia kuangua kilio ni kutokana na kwamba mara nyingi anakuwa na washiriki hao na ameshawazoea sasa aliposikia wanaaga shindano hilo aliumia sana.
 “Unajua wale washiriki ni kama rafiki zangu nimewazoea sana, wanapotajwa na majaji kuwa wanaaga shindano hilo, nilishindwa kujizuia na kujikuta machozi yakinitoka,” alisema Penny.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.