Josephine
Mushumbusi, mke wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Peter Slaa anadaiwa kula bata za hatari
nchini Marekani (United States of Amerika au U.S.A) akiwa na familia
yake, Amani limenyaka maisha yake nyuma ya pazia.
Ishu hiyo inakuja ikiwa ni siku chache
tangu Josephine alipoibua gumzo kubwa ndani na nje ya Bongo baada ya
kuanikwa mambo yake ya siri na Askofu wa Kanisa na Ufufuo na Uzima,
Josephat Gwajima akimtuhumu kumteka mumewe, Dk. Slaa na kumshawishi
kuachana na siasa.
ANASWA SEHEMU AKIJIDAI
Kwa mujibu wa Wabongo waishio nchini
humo (Diaspora), Josephine aliyetua nchini humo siku kadhaa zilizopita
akitokea Bongo na familia yake, amekuwa akinaswa sehemu mbalimbali
akijidai na kujiachia kwa raha zake.
“Mwacheni atulize machungu na maumivu
jamani. Kusema kweli amehangaika sana na Chadema na siasa za Tanzania
hivyo ameona bora ajiachie,” kilisema moja kati ya vyanzo vyetu na
kuongeza:
“Nafikiri huyu mama (Josephine) anaondoa
stress (mawazo) ya Gwajima na machungu ya kukosa u-first lady (mke wa
rais) baada ya mumewe (Dk. Slaa) kukosa nafasi ya kugombea urais ambayo
Chadema walimpa Edward Lowassa baada ya kujiunga na chama hicho.”
BATA MWANZO-MWISHO
Habari zilieleza kwamba, mwanzoni
mwanamama huyo alidaiwa kuonekana akila bata na kujiachia na rafiki zake
katika Jimbo la Maryland kabla ya kutimkia Indiana na wamekuwa
hawatulii jimbo moja kwani wameonekana pia huko Minnesota nchini
Marekani.
“Unajua wana marafiki kwenye majimbo mbalimbali hivyo hawatulii sehemu moja,” kilidai chanzo chetu.
MSIKIE JOSEPHINE
Akizungumza na gazeti moja nchini (siyo la Global) akiwa nchini humo juu ya maisha yake kwa sasa, Josephine alikaririwa akisema:
“You will see my fruits (utayaona mafanikio yangu). For the time being my hands are closed (kwa sasa nimefunga mikono yangu).
“Niruhusuni niendelee na maisha ya siasa
nje ya siasa. Majungu, propaganda nawaachia wahusika…sijaona issue
(jambo) lolote lenye content (maudhui) ya kujibu alichozungumza Gwajima.
“Am very busy now (sina nafasi kwa
sasa). And life is demanding too (na maisha yananihitaji pia), why
should I waste time with things which are not adding any value to me?
Thank you. (Kwanini nipoteze muda kwa vitu ambavyo haviniongezei thamani
yoyote? Asante).”
NINI KIFUATACHO?
Kwa mujibu wa Josephine, kwa sasa yeye
na Dk. Slaa wapo mapumzikoni nchini humo lakini wanajipanga kwa upande
mwingine wa kuwa wawekezaji na uwekezaji waliopanga baada ya kupewa
fedha na marafiki zao ni kujenga shule, hospitali na kuwawezesha
wanawake wajasiriamali pindi watakaporejea Bongo kutoka Marekani.


Note: Only a member of this blog may post a comment.