Saturday, September 26, 2015

Anonymous

MTIKILA Ampa Makavu LOWASSA.....Asema ni Mgonjwa na Tapeli...Adai Watanzania Wana Ugonjwa wa Unyani na Viongozi wa CHADEMA ni Wavuta Bangi

Mwenyekiti  wa  Chama  cha DP,Mchungaji Christopher Mtikila ,leo  asubuhi  alikuwa Live  Star Tv  katika  kipindi  cha Tuongee  Asubuhi  ambapo  ameongelea  mambo  mbalimbali  kama;
  1. Dhana ya ufisadi na aina za viongozi tunaohitaji kuwapatia Ikulu
  2. Umuhimu wa afya bora kwa wagombea uraisi
  3. Ahadi  za  CCM  na  CHADEMA  Kutoa  elimu  ya  bure
  4. Mapungufu  Ya  Edward Lowassa.
  5. Tafiti zilizofanywa na SYNOVATE  pamoja na TWAWEZA juu ya nani ana nafasi ya kushinda uraisi
Hapo  chini  kuna  video  za  maongezi  yake  ambazo  utapata  nafasi  ya  kuzisikiliza, lakini  kabla  ya  video  hizo, haya  ni  baadhi  ya  mambo  aliyoyaongea  Mtikila.

1-Sababu iliyofanya ngombea mwenza wake kutotokea ni dharura ya ugonjwa iliyompata mkewe huko Zanzibar na amesema Jumaatatu yake alienda ofisi za tume kufuatilia akaambiwa mwenyekiti Jaji Lubuva hajafika ofisini anaumwa hivyo akawaambia naye jaji Lubuva kwa kushindwa kuhudhuria ofisini kwa sababu ileile naye akatwe.

Amesema amepeleka kesi mahakama kuu na wiki ijayo ndio inatolewa uamuzi.

2. Mtikila amesema kafungua mashtaka kuzuia Lowasa kuendelea kugombea urais kwa hoja ya afya yake akijenga hoja kwamba muajiriwa yoyote lazima apime afya yake hivyo Lowasa anakosa sifa hiyo ya kupewa nchi.

3. Amesema watanzania tunaumwa epidomia, mwenyewe kauita  niunyani, yaani tukipewa kanga kofia viroba tunashabikia tu.
 
4. Amesema wanachama na viongozi wa chadema bangi na gongo kwao ni kama sakrament.

5.Amesema Lowassa ni tapeli kwa  kuwa  alitudanganya anaenda kutununulia mvua.

6. Alipoulizwa nani anamuona anaweza kuibadili Tanzania kati ya Lowassa na Magufuli alijibu Magufuli ndio sahihi japo ana mapungufu yake lakini zaidi yake yeye ndio anafaa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.