Klabu ya Simba SC September 20 imerejea katika uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kumkaribisha mgeni wake Kagera Sugar kutoka Bukoba, Simba ambayo imerejea kutokea Tanga ambapo ilicheza mechi zake mbili za awali katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga ambapo mechi ya kwanza ilicheza dhidi ya African Sports ya pili na Mgambo Shooting.
Simba imerejea kucheza mechi yake ya tatu uwanja wa Taifa Dar Es Salaam huku nahodha wao Mussa Hassan Mgosi akiwa jukwaani, Simba ambayo hadi sasa imecheza mechi mbili na kushinda zote. September 20 katika mechi dhidi ya Kagera Sugar, Simba imeibuka na ushindi wa jumla ya goli 3-1.
Hamisi Kiiza akishangilia goli lake kwa kusali
Magoli ya Simba yalifungwa kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Hamisi Kiiza dakika ya 30 baada ya kutumia vizuri krosi kutoka kwa Awadhi Juma. Kiiza alipachika magoli mengine mawili dakika ya 46 na 92 ya mchezo, huku Kagera Sugar wakiambulia goli moja peke lililofungwa na Mubaraka Yusuph dakika ya 60.
Nahodha wa Kagera Sugar George Kavilla akiwania mpira na Peter Mwalyanza
Hamisi Kiiza akidhibitiwa maridadi na mchezaji wa Kagera Sugar
Ibrahim Ajib akimpiga chenga beki wa Kagera Sugar
Simon Sserunkuma akidhibitiwa na beki wa Kagera Sugar
Salum Kanoni akimdhibiti Ibrahim Ajib
Hassan Kessy wa Simba akimdhibiti beki mwenzie wa Kagera Sugar asipite
Wachezaji wa Simba wakishangilia kwa pamoja goli la tatu la Kiiza
Haya ni matokeo ya Mechi zingine za Ligi Kuu zilizochezwa September 20
Mwadui FC 0 – 1 Azam FC
Mtibwa Sugar 2 – 1 Ndanda FC
Coastal Union 0 – 0 Toto Africans

Note: Only a member of this blog may post a comment.