WAKATI siku 32 zikiwa mbele kuufikia uchaguzi mkuu
Oktoba 25, mwaka huu, tegemeo kuu la mgombea urais wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa ni kutokea kwa mambo matano endapo
ataanguka kwenye kinyang’anyiro hicho, Uwazi limechimba.
Mgombea urais wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa.
Kwa mujibu wa mchambuzi mmoja wa mambo ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam ‘Mlimani’, Profesa Nathaniel Mlaumi, Lowassa ana siku
chache za maamuzi mengine endapo ataangushwa kwenye mbio za urais na
mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli.
MOJA
“Kwanza, kila mtu anajua kwamba, Ukawa una nguvu na umepata nguvu
zaidi baada ya Lowassa kuingia Chadema na wafuasi wengi.“Kama Lowassa
atashindwa kwenye uchaguzi Oktoba, hata Ukawa itasambaratika.
Haitakuwepo tena na maana ya Ukawa itakomea hapo. Naamini kama Lowassa
asingeingia Chadema, Ukawa hii ya leo ingeishia njiani.”
PILI
“Jambo la pili ni kupungua nguvu kwa Chadema. Kwa miaka yote nyuma,
Chadema kimekuwa kikizidi kuimarika kila baada ya uchaguzi, lakini mwaka
huu kitapungua nguvu.“Kitapungua nguvu kwa sababu, wana mpasuko wa
chini kwa chini lakini unazibwa na harakati za umoja kuelekea uchaguzi
mkuu wakiamini watachukua dola mwezi ujao. Kama nilivyosema Ukawa
itasambaratika. Hiyo itachangia kupungua nguvu kwa Chadema.”
TATU
“Lakini kuna jambo lingine la tatu. Lowassa ni mwanasiasa kwa sasa
lakini ili aendelee kuwa mwanasiasa ni lazima apate ushindi mwezi ujao.
Akishindwa, itabidi aachane na siasa kwa sababu, kwanza umri utakuwa
umekwenda.
“Kwa sasa ana miaka 62, kuja kugombea tena ni miaka mitano mbele ambapo
atakuwa na miaka 67. Atakuwa amechoka na hatakuwa na nafasi yoyote ndani
ya chama. Pia, kwa misukosuko hii ya kampeni, atakuwa amechoka sana na
atakabiliwa na mavune (uchovu baada ya shughuli nzito).”
“Nimekuwa nikikiangalia kwa umakini sana Chama Cha ACT-Wazalendo. Ni
chama chenye sera nzuri kwa sababu kinasimamia kupiga vita ufisadi.
Endapo Lowassa atashindwa kwenye uchaguzi ujao, kama nilivyosema awali,
Chadema kitapungua nguvu, hivyo ACT ndiyo chama kinachokuja kuwa kikubwa
cha upinzani hapa Tanzania.”
TANO
“Lakini pia kama Lowassa ataanguka, ina maana CCM itarudi madarakani
kwa sababu ndiyo chama tawala chenye nguvu katika kinyang’anyiro hiki
kikifuatiwa na Chadema.“Katika historia ya uchaguzi hapa Tanzania,
hakuna mwaka ambao CCM imewahi kupata wakati mgumu kama mwaka huu wa
2015. Nimewahi kuzungumza na kiongozi mmoja wa CCM wa ngazi ya juu,
aliniambia hata wao hawalali usingizi mwaka huu.
“Hii inatokana na ukweli kwamba, Lowassa kuhamia Chadema kumezidisha
ushindani. Kwa hiyo, kama Lowassa ataanguka, CCM kitajiimarisha zaidi
kuliko mwaka mwingine wowote. Hakitakubali kusimamia uzembe, kuangalia
makosa wala kulegea kwenye utekelezaji wa ilani zake.”
MWENENDO WA SIASA
Kuhusu mwenendo wa kisiasa nchini, mchambuzi huyo alisema
anasikitishwa na tabia za baadhi ya vyama kutengenezeana skendo ili
upande wa pili uonekane hovyo.
“Kuna watu walisema wamenasa ‘chating’ ya Mwigulu Nchemba, Januari
Makamba, Livingstone Lusinde (Kibajaj) na Angella Kairuki kwenye Mtandao
wa WhatsApp eti wakizungumzia mikakati ya kujipanga upya katika kampeni
kwa madai kwamba wanazidiwa na Lowassa.
“Hivi kwa akili za kawaida, Makamba ni naibu waziri wa mawasiliano na
teknolojia, anaweza kutumia mtandao kuzungumzia mambo hayo kweli? Tena
kwa kuchati badala ya kupiga?!
“Yale ni mambo ya kisiasa. Upande mmoja kutengeneza skendo ili kuuumiza upande mwingine. Ni hatari. Naviasa vyama vyote kuachana na siasa hizi za maji taka.”
“Yale ni mambo ya kisiasa. Upande mmoja kutengeneza skendo ili kuuumiza upande mwingine. Ni hatari. Naviasa vyama vyote kuachana na siasa hizi za maji taka.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.