Niwiki
nyingine tulivu kabisa tunakutana kupitia safu hii nikiamini kwamba
umzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama
kawaida.Leo mpenzi msomaji wangu nitazungumzia mambo ambayo mwanaume
anaweza kuyafanya katika kubaini kama mwanamke aliyenaye anafaa kuwa mke
au amuweke pembeni atafute mtu mwingine.
Nimeamua kuandika makala haya nikiamini kwamba, si kila unayeingia
naye kwenye uhusiano anafaa kuwa mkeo. Wengine ni pasua kichwa kiasi
kwamba ukijichanganya na kumuingiza ndani, yatakayokukuta utajuta.
Kimsingi vipo vimitihani vingi unaweza kumpa mpenzi wako lakini leo
nataka kukupa mitihani mitano ambayo ukimpa kisha akafaulu, huyo ana
kila sifa ya kuwa mkeo.
Moja; Siku ambayo umepanga aje kwako, hakikisha ndani kwako kuna nguo
chafu na vyombo vichafu. Uviweke katika mazingira ambayo ni rahisi yeye
akija kuviona. Sasa, kama atakuja na kuvikuta vyombo ni vichafu, nguo
zako pia ni chafu halafu yeye akawa hazungumzii suala ya kukufulia na
kukuoshea vyombo, huyo muangalie mara mbilimbili.
Mbili; Akija kwako, chukua simu yako kisha piga simu kama vile
unaongea na dada ambaye huwa anakuja hapo kwako kukufanyia usafi wa
nyumba, jifanye unamwambia kesho asichelewe kufika.
Endapo atasikia
mazungumzo yako halafu asiseme ‘baby mwambie tu kesho asije,
nitakupigia deki na kukusafishia nyumba’, huyo si ‘wife material’.
Tatu;
Ukijua kesho atakuja kwako, leo nenda kafanye ‘shopping’ ya vyakula
mbalimbali kama vile mchele, unga na mazagazaga mengine. Uhakikishe
vinakuwa katika mazingira ambayo ataviona.
Akishafika mpime kwa kumwambia kuwa, chakula kipo ila umeshindwa
kumuandalia hivyo muende hotelini mkale au uende ukamnunulie chipsi. Kwa
mwanamke ambaye anafaa kuwa mke, hapo atakuambia ‘noo baby, kwa kuwa
chakula kipo nitapika tule mpenzi. Lakini ukiona anasapoti suala la nyie
kwenda kununua chakula, huyo hafai kuwa mke.
Nne; Siku unamuahidi kumtoa ‘out’, akija kwako unajifanya umekosa
amani ghafla na akikuuliza unamwambia kuwa, mama yako anaumwa sana na
pesa uliyonayo ndiyo ambayo uliipigia mahesabu ya kwenda kuitumia out.
Akipuuza kuumwa kwa mama yako na kusisitiza muende tu ‘out’ huku
akikuambia kuwa ndugu zako wengine watamsaidia, huyo ana walakini.
Tano; Akikutembelea kwako, yeye akiwa sebuleni muwashie TV kisha wewe
anza kupika ukimuandalia chakula. Katika mazingira ya kawaida anatakiwa
achukue nafasi yake kama mke mtarajiwa lakini akikuacha wewe upike
kisha yeye akaendelea kuangalia TV kwa mbwembwe, hapo hamna mke.
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo wewe mwanaume unaweza kuyafanya katika
kumtesti mpenzi wako kama anafaa kuwa mkeo.Angalizo; kwenye mapenzi
usanii ni mwingi mno, wapo ambao wanaweza kujifanyisha sana. Yaani
ukampa mitihani hiyo na akafaulu vizuri kabisa lakini ukashangaa
ukishamuweka ndani anaanza kukufanyia vitu vya tofauti.
Tuonane wiki ijayo.
Friday, September 4, 2015
MAMBO MA-5 YA KUMTESTI MPENZI KAMA ANAFAA KUWA MKE!
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Filed Under:
MAPENZI
on Friday, September 4, 2015

Note: Only a member of this blog may post a comment.