Dustan Shekidele, Moro
Mfanyakazi wa ndani ‘hausigeli’ mmoja mkoani hapa
aliyefahamika kwa jina moja la Rehema (16) ambaye alifanya kazi hiyo kwa
wiki moja, akimshikia mwenzake aliyekwenda kijijini kwao lfakara
wilayani Kilombero kumuuguza mama yake, amejifungia chumbani kisha
kujinyonga kwa kutumia kanga.
Tukio hilo la kuhuzunisha lilijiri usiku wa kuamkia juzi (Alhamisi)
kwenye nyumba namba 17\l3 aliyokuwa akifanya kazi Rehema iliyopo Mtaa wa
Kazingwa Kata ya Kiwanja Cha Ndege mjini hapa huku kisa kikiwa cha
kusikitisha cha kimapenzi.
Kwa mujibu wa mashuhuda, katika hali ya kushangaza, familia
iliyokumbwa na mkasa huo iligoma kuhojiwa na mwandishi wetu huku
wakimtaka akachukue maelezo polisi.
Baada ya wanafamilia hao kugoma, mwanahabari wetu alizungumza na mmoja wa wapangaji aliyeomba hifadhi ya jina ambaye alisimulia:
“Kweli akamleta huyu Rehema. Cha ajabu Alhamisi, majira ya saa 1:00 asubuhi anagongewa mlango wa chumba ila hakujibu chochote.
Baadhi ya mashuhuda wengine walieleza kwamba hadi Rehema anachukua
uamuzi huo inawezekana kuna mambo yalikuwa yamemfika shingoni.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa mtaa huo, Mohamed Mbega alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambapo aliita polisi waliofika na kuuchukua mwili
wa marehemu Rehema kwa uchunguzi zaidi na taratibu za mazishi.
Katika tukio hilo lililokusanya umati mkubwa, Rehema hakuacha ujumbe
wowote kwani begi lake lilikaguliwa na halikuwa na ujumbe zaidi ya nguo
zake hivyo kumfanya bosi wake kuchanganyikiwa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.