Wednesday, September 23, 2015

Anonymous

LOWASSA Chali Mbele ya MAGUFULI!

Taasisi ya Twaweza imetoa utafiti wake ambao inasema imefanya kwa wananchi wa Tanzania bara kutoka mikoa tofauti ya Tanzania.
Swali la kama uchaguzi ungefanyika leo, ungempigia kura mgombea wa chama gani? Wanasema watu wamejibu kama ifuatavyo

CCM - 66%
CHADEMA - 22%
CUF - 1%
ACT wazalendo - 0%
UKAWA - 3%
Kingine - 6%
Hakuna jibu 2%

Utafiti huo  uliotokana na kuhoji watu 1848 kutoka mikoa tofauti ya Tanzania bara, inasema iliwauliza wananchi hao: Ukimwacha Rais Kikwete, iwapo uchaguzi wa urais ungefanyika leo, ungemchagua nani?

...Majibu ya swali hilo TWAWEZA wanasema limejibiwa na wananchi hao kama ifuatavyo

Magufuli 65 %
Lowassa 25%
Mwingine 3%
Sijui/kataa jibu 7%

Akitangaza utafiti huo leo, Mkurugenzi mtendaji wa TWAWEZA,  Aidan Eiyakuze  amesema kwa upande wa ubunge, Utafiti huo unaonyesha kuwa CCM inaongeza kwa asilimia 60 na kufuatiwa na CHADEMA asilimia 26. 

Je, unakubaliana na utafiti huu?! Toa maoni yako hapa chini

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.