Miss
Tanzania 2014/15 Lilian Kamazima akitolewa damu kwaajili ya kuhamasisha
jamii katika suala la uchangiaji damu safi na salama kwenye kituo cha
Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Kamazima akitolewa damu ndani ya Viwanja vya Mnazi mmoja.
Lilian akiwa ameshikilia damu hiyo muda mufupi baada ya kuhitimisha zoezi hilo la kuchangia damu safi na salama.
Mmoja
wa wauguzi katika kitengo cha damu safi na salama akiwa katika pozi na
Miss Tanzania Lilian Kamazima muda mfupi baada ya kumaliza kutoa damu.
Na Musa Mateja
MISS Tanzania 2014/15 Lilian Kamazima
jana aliweza kuchangia damu salama katika kituo cha Mnazi mmoja jijini
Dar es Salaam, ikiwa ni moja ya huduma ya kuchangia jamii kabla ya
kuanza safari yake ya kuelekea kwenye shindano la Miss World 2015
linalotarajiwa kufanyika nchini China hivi karibuni.
Akizungumzia tukio hilo la kuchangia
damu alisema kwamba, ameguswa na kuamua kutoa damu yake ili kuchangia
baadhi ya Watanzania wenye matatizo na hasa ambao wamekuwa wakipoteza
maisha yao kwakukosa damu safi na salama.
“Mimi kama miss Tanzania ni jukumu langu
kuhakikisha nawahamasisha Watanzania wote kushiriki kwenye mambo ya
kijamii mbalimbali likiwemo na hili la uchangiaji damu safi na salama,
lakini kufanya hivyo pia ni moja mambo muhimu ambayo napaswa kuyafanya
kabla siajaenda kuungana na warimbwende wenzangu mwezi wa kumi na moja
tutakapokua kwenye mashindano hayo,” alisema Kamazima.
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL.

Note: Only a member of this blog may post a comment.