WIKIENDI nyingine Mapaparazi Wetu, Richard Bukos ‘Mpigapicha Mkuu’, Musa Mateja ‘Toz’ na Dustan Shekidele ‘Mzee wa Mji Kasoro Bahari’ walijiachia katika viwanja tofauti kusaka matukio huku wakiwasiliana na mkuu wao aliyekuwa makao makuu ya gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
Mkuu akiwa katika kiti chake cha kunesanesa, anaangalia saa ukutani na kugundua mida tayari imesonga, ni saa mbili na nusu usiku. Anamtwangia Bukos aliyekuwa Biharamulo kwenye kampeni za Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli.
Saa 2:31
AKURUPUKA GESTI KUONA MWANAMKE ANA MGUU MMOJA
Makao Makuu: Haya niambie Bukos, uko wapi na mnaendeleaje na ziara za Dk. Magufuli huko mikoani?
Bukos: Mkuu leo ndiyo tumemaliza Mkoa wa Kigoma, Mzee wa Selema amemaliza kampeni zake Kakonko, tukaingia Mkoa wa Kagera napo kama kawa, mzee akafanya yake Biharamulo kisha tukaja Mkoa wa Geita na usiku huu tumejipumzisha eneo la Katoro wilayani Chato.
Makao Makuu: Vipi kuna kituko umekinasa?
Mkuu: Kuna mchimba madini alizoa changu akaingia naye gesti jirani na tulipofikia sasa wakati wa maandalizi yule changu kumbe alikuwa na mguu mmoja wa bandia, jamaa alipokwenda bafuni changu akauvua, wakati anatoka bafuni na kumshtukia mwanamke aliyenaye ana paja ‘kipisi’, pombe zote zilimtoka nahisi alifikiri jini akaanza kupiga mayowe na kuchomoka gesti nduki na kumuachia chumba.
Makao Makuu: Kwani jamaa hakumjua kama ana tatizo la mguu?
Bukos: Mkuu si unajua jamaa mwenyewe mlevi halafu huyu changu naye ni mjanja sana anatembea kistaili f’lani kama madoido kumbe anaficha ulemavu.
Makao Makuu: Poa Bukos, ngoja nimtafute Mzee wa Mji Kasoro Bahari, Dustan Shekidele.
Saa 4:00
MUME WA MTU AKUTWA GESTI NA DENTI
Makao Makuu: Shekidele habari ya leo?
Shekidele: Mkuu sijambo na mishe zinakwenda kama kawaida.
Makao Makuu: Leta maneno upo wapi na nini umekinasa hadi wakati huu?
Shekidele: Nipo hapa Mji Mpya katika Ukumbi wa Samaki Sport kuna tukio kabambe limetokea.
Makao Makuu: Shekidele unazunguka sana, leta utamu.
Shekidele: Mkuu usiwe na shaka, hapa nakupa ile kitu roho inapenda. Ni hivi, kuna jamaa alikuwa na kadenti ka’sekondari akazama nako gesti sasa bahati haikuwa yake. Ile anazama kuna polisi jamii walikuwa wamekaa jirani na mlango wa gesti hivyo walipomuona denti akiwa na nguo za shule anaingia gesti na mtu mzima, wakamuibukia.
Makao Makuu: Duuh! Hiyo hatari!
Shekidele: Polisi hao jamii walimuamuru mhudumu awaoneshe chumba walichoingia, walipoingia wamewakuta wameketi kitandani, wote wamepigwa butwaa!
Makao Makuu: Yaani hiyo muvi sitaki iishe. Enhe!
Shekidele: Sasa ndiyo wametafuta majina katika simu ya huyu njembe na kukuta namba ya mkewe hivyo wamempigia na wanawapeleka wote nyumbani kwa mkewe huko Kihonda.
Makao Makuu: Hahaha huyo leo kaumbuka, fuatilia hatua kwa hatua halafu utatutumia picha ili tulirushe hewani tukio hilo jamii ipate kumuona mwaribifu wa madenti.
Saa 7:00
WAREMBO WAZICHAPA KISA MAGUFULI, LOWASSA
Makao Makuu: Mambo kijana wangu, uliniambia upo Tegeta, unaweza kuniambia mambo yakoje hapo?
Mateja: Mkuu ni kweli unachokiongea kwa sasa nipo Tegeta narudi zangu ‘home’ ingawa kuna tukio nimelishuhudia laivu hapa nimebaki nimeduwaa maana kama mwendo ndiyo huu basi siasa za mwaka huu zisipokemewa zinaweza kutuletea machafuko.
Makao Makuu: Duuh, mbona unanitisha kuna jambo gani la ajabu?
Mateja: Mkuu nikiwa mitaa ya Kawe nimekuta akina dada wamekunjana eti kisa siasa.
Makao Makuu: Khaaa! Kisa ni kipi hasa ulivyosikia?
Mateja: Naambiwa hawa wadada wameshushwa kwenye daladala la kutoka Kariakoo sababu walianza kubishana mmoja anasema anampenda Magufuli kwa kuwa mchapakazi sasa sijui akaanza kuizungumzia afya ya Lowassa ndipo hali ilipotibuka. Huyu mwenzake mfuasi wa Lowassa hakufurahishwa na kauli hiyo ndipo wakaanza kubishana kisha kuzichapa kavukavu.
Makao Makuu: Mmmh… kweli kwa hali hiyo mwaka huu kuna kimbembe cha maana, eeh imekuwaje?
Mateja: Wasamaria wema walipoona wataumizana wamewaamulia na kuwataka kila mmoja aendelee na safari yake, wameondoka huku wakirushiana maneno makali na kusema watakutana Oktoba 25 siku ya uchaguzi ndiyo kitajulikana kama rais atakuwa Lowassa au Magufuli.
Makao Makuu: Duuh ya leo kali, poa Mateja piga kazi ila muda umeenda hivyo uwaambie wenzako mkalale.
Mateja: Sawa Mkuu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.