Imelda Mtema
KIMENUKA tena! Katika kile kinachoonekana kama ni
kejeli kwa shosti wake wa zamani, ambaye sasa picha hazipandi, staa wa
filamu Kajala Masanja, mwishoni mwa wiki iliyopita alimmwagia ‘minoti’
mingi Zarinah Hassan ‘Zari’ wakati wa hafla ya kutimiza siku 40 tangu
kuzaliwa kwa mtoto wake Tiffah.
Mwigizaji Kajala Masanja pamoja na shoga yake wakiwa kwenye shughuli hiyo.
Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwa
Diamond, mitaa ya Madale-Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu.
Ilikuwa ni wakati Zari, alipokuwa
akicheza muziki huku akipokea zawadi kutoka kwa waalikwa, ndipo
muigizaji huyo, alipotumia zaidi ya dakika 20 kummwagia minoti ya
shilingi elfu kumikumi. Baadhi ya watu waliohudhuria shughuli hiyo
waliweka kipande cha video ya Kajala akifanya mambo yake kwenye mitandao
ya intaneti na mara moja, Wema akakiona.
Zari akiwa na mzazi mwenzake pamoja na mtoto wao.
inadaiwa kuwa kitendo hicho kilimkera na
alipowasiliana na gazeti hili alisema. “Hata kama ni kweli tumegombana,
bado yeye hakutakiwa kufanya vile, ilionekana anataka kunisanifu tu,
kama kweli Kajala anasema kwa watu kila siku kuwa mimi ni rafiki yake na
hawezi kuifuta tattoo yangu aliyojichora, asingeweza kufanya kitu kama
hicho.
Sasa mwambieni kabisa kama ni hivyo,
aifute mara moja ile tattoo,” alisema kwa kifupi, akionekana kukasirika.
Risasi Mchanganyiko lilipomtafuta Kajala na kummegea ‘ubuyu’ huo, naye
bila kupepesa macho alitiririka; “Mimi nilienda kumtunza Zari kama
waalikwa wengine walivyofanya, kama yeye anaona sikufanya vizuri mimi
hainihusu, na kama anaweza kuifuta hii tattoo aje tu aifute, haina
shida.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.