Beef la Soundcity TV na P Square ikiwemo manager wao Jude Okoye bado linaendelea na pengine litaendelea kwa muda mrefu.
Soundcity TV imekerekwa na kauli ya manager wa P Square Jude Okoye iliyosema kuwa; “nyinyi mnapata mamilioni ya pesa lakini wasanii hawalipwi fungu lao kwenye hayo mamilioni”… kwa hasira wamepost picha inayoonyesha kama kumshushia heshima manager wa P Square na kuandika ujumbe mrefu sana kujibu tuhuma hizo…
Cha kwanza ambacho Soundcity TV imesema ni kwamba wanatambua kuwa hawawapi P Square favour yoyote kwani wakiwa na kazi nzuri na wakiileta kwenye kituo hicho, Soundcity haitakiwi
kuikataa bali kuipromote kazi hiyo kwenye platform mbalimbali
walizonazo kwani kusupport kazi za wasanii sio ombi la msanii bali ni
jukumu lao.
Kuhusu kutokulipa wasanii fungu lao Soundcity TV wamekataa
kabisa kitendo hiki na wamesisitiza kuwa kazi ya manager ni kupokea na
kuthibitisha kuwa amepokea ile asilimia yake na ya msanii iliyotokana na
wimbo wao kupigwa kwenye kituo hicho cha TV…
>>>“Kazi
yako kama manager ni kuhakikisha wasanii wako wanapata mafungu yao
kutokana na kazi zao kuchezwa kwenye TV, ukifuatilia kupitia COSON, MSCN
utagundua kuwa SOUNDCITY inawalipa wasanii mafungu yao kila mwaka…
COSON ni Chama cha Haki Miliki Nigeria na MSCN ni Chama cha Haki Miliki
na Muziki Nigeria, pengine ungeweza kujifunza zaidi kuhusu hivi vitu
viwili kupita tovuti yao http://www.cosonng.com… <<< SOUNDCITY.
Soundcity Tv wameendelea kusema…
>>>
“Mnasema mna haki ya kuchagua kama mnataka kufanya kazi na brand yetu
au la na mmechagua kutokufanya kazi na sisi ,mko sahihi na sisi pia tuna
haki hiyo hiyo kwahiyo na sisi tunachagua kutokufanya kazi na nyie na
kuanzia leo video zenu hazitakuwa zinapatikana kwenye mtandao wala
channel yetu na pia kuanzia leo tunajivua majukumu yote ya kibiashara na
nyie… mmefanya maamuzi na sisi pia tumechukua hatua hiyo, Simple!” <<< SOUNDCITY.

Note: Only a member of this blog may post a comment.