Tuesday, September 22, 2015

Anonymous

Kambi ya MAGUFULI!, UKAWA & CCM Mashindano? LOWASSA na gesi +TWAWEZA na Utafiti wa Siasa… (Audio).

Uchambuzi wa magazeti leo Jumanne 22 September 2015 @CloudsFM umekupita? Ninazo hapa zile kubwa kwenye vichwa vya habari asubuhi hii, kama zilikupita karibu ucheki na hizi nyingine hapa chini.
Matajiri watano kuibeba UKAWA, hujuma nzito ndani ya kambi ya Dk John Magufuli, Edward Lowassa kupitia mikataba ya gesi, CCM kwenda likizo ya lazima, Mgombea Urais CHADEMA Edward Lowassa asema wananchi wasiogope vitisho. 

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe asema chama chake kina watu watano wenye uwezo wa kukibeba chama hicho kwenye shughuli zao za Kampeni, Edward Lowassa ameahidi kujenga kamati maalumu ili kuchunguza mikataba ya gesi na Dk John Magufuli ameendelea kukosoa awamu za Serikali zilizopita akikumbushia Ranchi zilizouzwa kwa kukeuka taratibu. 

UKAWA na CCM washindana kujaza watu kwenye mikutano yao ya Kampeni huku CCM wasema ushindi wa jukwani ni kwa asilimia 30%  huku ushindi mwingine ni mbinu, Taasisi ya TWAWEZA kutangaza matokeo yake ya utafiti wa hali ya Siasa nchini kupitia ‘Sauti ya Mwananchi’, utafiti utakao baini wananchi wanataka Chama gani. 

Wagonjwa wa kipindupindu wafika 959, Watalii 9 kati ya 20 waliokwama kwenye moto wa Mlima Meru waokolewa jana na Mamlaka ya Hifadhi Tanzania TANAPA… Serikali imeridhishwa na mchakato wa kuanzisha Chuo Kikuu cha Hesabu na Sayansi Bagamoyo.
Sauti yote ya uchambuzi wa magazeti kwenye #PowerBreakfast ninayo tayari hapa chini, bonyeza play kuisikiliza moja kwa moja.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.